25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

MCHECHU WA NHC ASIMAMISHWA KAZI

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi

Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu ili kupisha uchunguzi.

Mbali na Mchechu, Lukuvi pia ameagiza bodi ya shirika hilo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Huduma za Mikoa na Utawala, Raymond Mndolwa.

Taarifa iliyotolewa jana saa moja usiku na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – Maelezo na Msemaji wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi, ilieleza kuwa Lukuvi amechukua uamuzi huo kutokana na mamlaka aliyopewa chini ya kifungu F. 35 (1) cha Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2009.

Abbasi akikariri taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dorothy Mwanyika, ambaye alisisitiza kuwa uamuzi huo unapaswa kutekelezwa kuanzia jana ili kupisha tuhuma zinazowakabili watendaji hao.

Ingawa taarifa hiyo haikuzitaja tuhuma zinazowakabili Mchechu na Mndolwa, katikati ya wiki hii wakati Rais Dk. John Magufuli akizindua nyumba mpya 150 za makazi zilizojengwa na NHC eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma, alimshushia tuhuma nzito Mchechu na shirika analoliongoza na kumtaka aketi na Waziri Lukuvi na kufanya uchambuzi juu ya mahali walipokosea na watakaporekebisha kuyapeleka mapendekezo ambayo yana uhalisia.

Tuhuma hizo ni pamoja na kuwapo na kutoelewana baina yao, kutumiwa na wanasiasa kwa malengo fulani, matumizi na miradi inayotia shaka na kufanya kazi zinazogongana na shirika wanaloliongoza.

“NHC mjitathimini, muende kwenye direction (mwelekeo) ninayoitaka, ili tunafika kukopesha tukopeshe tukijua hizi ni kwa ajili ya kujenga nyumba, ni kwa ajili ya manufaa ya Shirika la Nyumba,” alisema Rais Magufuli.

Kwa habari kamili nunua nakala yako ya MTANZANIA

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles