24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge wa Chadema alazwa Muhimbili

Mbunge wa viti Maalum kwa tiketi ya  CHADEMA, Maulida Anna Komu
Mbunge wa viti Maalum kwa tiketi ya CHADEMA, Maulida Anna Komu

Hadia Khamis na Jonas Mushi, Dar es Salaam

MBUNGE wa viti Maalum kwa tiketi ya  CHADEMA, Maulida Anna Komu, amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa   wiki mbili sasa.

Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbil,i Dorris Ishenda, alisema jana kuwa Komu alifikishwa hospitalini hapo   wiki iliyopita na  kulazwa katika wodi ya magonjwa ya moyo.

“Ni kweli amelazwa katika wodi ya magonjwa ya moyo kwa ajili ya matibabu na hali yake inaendelea vizuri,”alisema Ishenda.

Mtanzania lilipotaka kufahamu anasumbuliwa na tatizo gani Ishenda alisema ugonjwa ni siri kati ya daktari na mgonjwa mwenyewe hivyo hawezi kulizungumzia  hilo.

“Labda ndugu ndiyo wanaweza kukwambia anasumbuliwa na nini, mimi kama ofisa wa habari siruhusiwi kisheria kuzungumza ugonjwa wa mtu kwani ni siri baina ya daktari na mgonjwa mwenyewe,”alisema  Ishenda.

Akizungumzia hali ya Brigedia Jeneral (Mstaafu) Hashim Mbita, Ishenda alisema bado yupo chini ya uangalizi maalum wa daktari (ICU) kwa ajili ya matibabu.

Alisema  hali yake siyo mbaya sana na wala siyo nzuri sana na timu ya madaktari wanafanya jitihada za kuhakikisha   anarudi katika hali yake ya kawaida.

Brigedia Jenerali Mbita alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili  zaidi ya  mwezi mmoja  na nusu sasa kwa ajili ya matibabu.

Awali alilazwa katika wodi ya magonjwa ya moyo kabla ya kuhamishiwa   ICU.

Wakati huhuo Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inatarajia kuweka kambi maalum ikiwa ni pamoja na kujenga mahema kwa ajili ya uchunguzi kwa mgonjwa atakayebainika kuwa na ugonjwa wa Ebola. Kambi hiyo inatarajiwa kuwekwa mapema wiki hii.

Mapema wiki hii, baadhi ya madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili walipewa mafunzo ya jinsi ya kumhudumia mgonjwa wa Ebola.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles