30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE ATAKA WANAOEGESHA MAGARI OVYO WACHUKULIWE HATUA

NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

MBUNGE wa Kiembe Samaki (CCM), Ibrahimu Hassanal Mohammed amehoji ni lini serikali itawachukulia hatua watu wanaoegesha magari ovyo.

Alisema watu wa aina hiyo husababisha adha kwa watu wengine hasa nyakati za usiku katika Jiji la Dar es Salaam.

Kiuliza swali hilo jana, Mohammed   alisema jiji hlo umekuwa kama vile hauna sheria kwa sababu ya watu  kuegesha magari ovyo.

“ Watu wenye maduka waliopewa kibali cha kuegesha magari yao kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 11 jioni wameonekana wakihodhi nafasi hiyo kwa saa 24.

Je ni lini watu wenye tabia hiyo watachukuliwa hatua za  sheria?” alihoji Mbunge huyo.

Akimjibu,   Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo alisema sheria ndogo ya maegesho ya magari GN.Na.60 ya mwaka 1998 kifungu cha 6(1) inaipa mamlaka Halmashauri ya Jiji   kudhibiti na kusimamia maeneo ya maegesho ya magari yanayoruhusiwa kwa mujibu wa sheria.

Alisema   sheria hiyo inaondoa kero, usumbufu na msongamano katika mitaa na barabara za umma.

“Kwa mujibu wa sheria hiyo, maegesho yote ya magari ya kulipia na maegesho yaliyohifadhiwa yanatumika kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 12 jioni,”alisema Jafo.

Alisema baada ya muda huo maeneo hayo huwa huru kwa matumizi ya umma  na   itakapobainika mtu kuhodhi maeneo hayo baada ya saa 12 jioni, Halmashari ya Jiji huchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

‘’Kazi ya ukaguzi na udhibiti wa maeneo ya maegesho imetolewa kwa mawakala katika Jiji hilo.

“Natoa wito kwa wamiliki wote wa magari kuacha kuegesha magari bila utaratibu hasa wakati wa usiku na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine,’’ alisema Jafo

Naibu Waziri alisema serikali haitasita kuwachukulia hatua kali kwa wote watakaobainika kukiuka taratibu za maegesho ya magari katika jiji hilo kwa sababu kufanya hivyo ni kusababisha msongamano na kero kubwa kwa wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles