26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mbowe, Matiko wakata rufaa kupinga kufutiwa dhamana

Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wamekata rufaa kupinga uamuzi wa kufutiwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Leo Ijumaa Novemba 23, Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri wa mahakama hiyo, alitoa uamuzi wa kuwafutia dhamana washtakiwa hao kwa kukiuka masharti ya dhamana.

Amesema hoja za viongozi hao kutokuwepo mahakamani hapo wakati shauri lao lilipokuja kutajwa hazina mashiko.

“Sababu zinazotolewa wadhamini pamoja na Mbowe mwenyewe za kutohudhuria mahakamani zinapishana, hivyo basi nimeamua kuwafutia dhamana zao,” amesema Hakimu Mashauri.

Mara baada ya kutoa uamuzi huo, Wakili wa washtakiwa hao Peter Kibatala ameiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi ili kusubiri rufaa ya kupinga uamuzi wa kufutiwa dhamana kwa viongozi hao.

Hata hivyo hoja hiyo ilipingwa na Wakili wa Jamhuri, Faraja Nchimbi, ambapo alisema kuwa hoja ya Kibatala haina mashiko na kuitaka mahakama hiyo kutupilia mbali.

Hata hivyo Hakimu Mashauri aliahirisha shauri hilo hadi saa 7:30 mchana ili atoe uamuzi wa kuendelea na shauri hilo kwa hatua ya usikilizaji au la.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles