27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

MBOWE: DEREVA WA LISSU ANAPATIWA MATIBABU YA KISAIKOLOJIA

Dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, Simon Bakari, yuko nchini Kenya akipatiwa matibabu ya kisaikolojia katika Hospitali ya Nairobi aliyolazwa Lissu.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amebainisha hayo leo Septemba 10, ikiwa ni siku moja baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto kumtaka dereva huyo kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kama alivyofanya kwa gazeti la MTANZANIA toleo la jana Jumamosi.

Katika taarifa yake aliyotoa jijini Nairobi, nchini Kenya, Mbowe amesema dereva huyo anapatiwa huduma hiyo kutokana na kushuhudia shambulio la Lissu kupigwa risasi na kujeruhiwa ambapo yeye aliokoka kimiujiza.

“Anasumbuliwa na msongo mkubwa wa mawazo. Naye hatukuona busara kuendelea kumwacha nchini hadi hapo hali yake ya kiafya na kiusalama itakapohakikishwa, ni dhahiri kwa aina ya shambulio lilivyokuwa, wauaji walikusudia kuwaua wote, Lissu na dereva wake.

“Hofu kuu ya usalama wa Lissu na dereva wake ilitanda kote nchini Tanzania baada ya shambulio dhidi ya uhai wao kushindwa kufanikiwa. Busara ya ki-usalama ilitulazimisha kuwatoa waathirika nje ya mipaka ya nchi hadi hapo usalama wao utakapohakikishwa,” amesema Mbowe.

Katika hatua nyingine, Mbowe amesema maisha ya Lissu yalikuwa hatarini ambapo yalihitajika matibabu maalumu na  ya haraka kutoka kwa Madaktari Bingwa wa kutosha sambamba na vifaa tiba visivyo na shaka yoyote ili kuokoa maisha yake baada ya kazi kubwa na ya kupongezwa ya awali iliyofanywa na madaktari kadhaa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Aidha, amesema upande wa Uongozi wa Bunge na Serikali ulisisitiza Lissu apelekwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kama sivyo hawatakuwa tayari kubeba gharama yeyote inayohusiana na matibabu yake lakini upande wake na wabunge wa Umoja qa Katiba ya Watanzania (Ukawa), ulisisitiza apelekwe moja kwa moja Nairobi na kama Bunge na Serikali hawatakuwa tayari kubeba gharama za kuokoa maisha yake basi Chadema na Watanzania wenye mapenzi mema watachangia gharama hizo za kuokoa maisha kitibabu na kiusalama.

Hata hivyo, Mbowe amesema hali ya Lissu inaendelea vizuri ambapo tangu afikishwe hospitalini hapo usiku wa Septemba 7,  kazi kubwa ya kuendelea kuokoa maisha yake ilifanywa usiku kucha na jopo la madaktari wasiopungua 10 lakini changamoto iliyopo ni matibabu yake ambayo ni maalumu na yanahitaji wataalamu wengi, vifaa tiba maalumu na gharama kubwa ambapo hadi sasa, zaidi ya Sh millioni 100 zimeshatumika kuokoa yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles