33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MBINU ZA KUEPUKA KUNUKA KIKWAPA

lemon_wedges

Na MWANDISHI WETU, 

VIJANA wanapofikia umri wa kubalehe, moja kati ya dalili wanazokumbana nazo ni kuota nywele sehemu za siri ikiwamo kwapani. Wengi wao wamekuwa wakishindwa kujiweka katika hali ya usafi hivyo kujikuta wakitoa harufu kali ya jasho.

Jambo hilo huwakwaza watu wengi na hivyo kujikuta wakitengwa bila kujua sababu.

Kunuka kikwapa  ni  tatizo kubwa katika mwili wa binadamu. Tatizo hili husababishwa na bakteria wanaovutiwa na jasho au unyevunyevu chini ya kwapa.
Sasa basi, kuna njia nyingi ambazo watu wengi huzitumia ili kwapa liwe na harufu nzuri, kavu na safi.

Wengine hutumia njia za kisasa ambazo ni pamoja na kupaka doodoranti au pafyumu zinazosaidia kuondoa harufu mbaya mwilini.

Lakini kama hiyo haitoshi, kuna njia za kisasa zinazoweza kuzuia harufu ya kwapa ambazo ni pamoja na kupaka kipande cha limao kwenye kwapa na kuacha lipate hewa  safi ili kuua vijidudu na kutoa tezi za jasho kuondoa harufu mbaya.

Kuvaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufi zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kuwa kavu, safi na bila harufu mbaya.

Kuoga kila siku na kusafisha nguo kwa maji safi kunasaidia kuua bakteria na ambao husababisha harufu mbaya.

Pia kunywa maji mengi kila siku kunakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa.

Njia nyingine inayoshauriwa ni kuhakikisha kuwa unaosha kwapa mara kwa mara kwa kutumia sabuni zenye dawa (medicated soaps).

Aidha, kupunguza kula chakula chenye viungo vingi hasa vitunguu. Inasemekana kuwa kula vitunguu vingi kunachangia mwili kutoa harufu kali.

Licha ya pafyumu na spray kusaidia kuondoa harufu mbaya mwilini, hii si dawa endelevu kwani baada ya muda harufu inaweza kurudi palepale hivyo ni vema kutumia njia za asili kukabiliana na hali hiyo. Pafyumu haiwezi kutibu tatizo moja kwa moja.

Pia inashauriwa kuwa baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao huwavutia bakteria kukua katika maeneo yaliyojificha (yenye mikunjo).

Mbinu nyingine ni kujitahidi kunyoa nywele za kwapa mara kwa mara na kuepuka kukaa sehemu zenye joto kupita kiasi kwa muda mrefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles