21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

Mbeya Kwanza yaweka rekodi, Azam yabanwa Mkwakwani

Na Daines Msumeno,TUDARCo


Ligi Kuu Tanzania Bara imeanza rasmi leo, Septemba 27, 2021 kwa michezo mitatu kupigwa kwenye viwanja tofauti, huku Mbeya Kwanza ikiweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kufunga bao msimu huu wa 2021/2022.


Mbeya Kwanza ambayo ni timu mpya Ligi Kuu, imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar bao lilifungwa na mchezaji William Egdar dakika ya 50 kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.


Mchezo huo ndiyo ulikuwa wa kwanza ambao ulipigwa majira ya saa 8:00 mchana, wakati mingine miwili ilianza saa 10:00 jioni.


Bao la pili msimu huu limefungwa na Shiza Kichuya dakika ya 13, Namungo ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold, huku bao la pili likifungwa na Reliants Lusajo dakika ya 81 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.


Mchezo mwingine Azam FC na Coastal Union zimetoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Mkwakwani,jijini Tanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles