24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Mbeya City yamnasa beki wa Yanga

Rajab Zahir
Mbeya City yamnasa beki wa Yanga

Na WINFRIDA NGONYANI -DAR ES SALAAM

BEKI wa zamani wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Rajab Zahir, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea timu ya Mbeya City katika msimu ujao wa ligi.

Zahir alikuwa akicheza kwa mkopo katika kikosi cha Stand United ya Shinyanga akitokea Yanga, lakini  amejiunga na Mbeya City baada ya kukosa nafasi ya kucheza chini ya kocha mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans van der Pluijm.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Mbeya City, Dismas Ten, alisema Zahir amesajiliwa ili kukiongezea nguvu kikosi hicho kinachonolewa na kocha, Kinnah Phiri raia wa Malawi.

“Tumemsajili Zahir tukiamini kuwa ni beki ambaye atatufaa kwenye safu ya ulinzi msimu ujao, kocha ameridhia ujio wake hivyo atajiunga na wenzake mazoezini na kujiandaa na michezo ya kirafiki ambayo tutacheza,” alisema.

Hivi karibuni Mbeya City ambayo imejichimbia mjini Kyela, ilifanikiwa pia kunasa saini ya aliyekuwa mshambuliaji wa kutumainiwa wa Tanzania Prisons, Mohamed Mkopi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles