27.6 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mbaroni kwa utoaji tiketi feki mwendokasi

Na Bakari Kimwanga-DAR ES SALAAM


WAKUSANYA fedha zaidi 50 wa Kituo Cha Mabasi Yaendeyo Haraka (DART), vituo cha Kimara na Gerezani jijini Dar es Salaam wametiwa mbaroni na jeshi la polisi kwa tuhuma za kutoa tiketi feki kwa abiri unaotumia mabasi hayo.

Hatua hiyo imekuja baada ya MTANZANIA katika ripoti yake maalumu Juni mwaka huu, kuhusu usafiri wa mabasi hayo namna wajanja wanavyotumia mwanya wa kutokusanya mapato kieletroniki na kusababisha hasara kwa serikali kukosa mapato yake stahiki.

Suala la ukusanyaji wa mapato ni moja ya msisitizo wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dk. John Magufuli ambaye kila mara amekuwa akikazia umuhimu wa agizo lake la kuwa na wawekezaji wanaofuata sheria  za nchi.

Chanzo cha kuaminika kiliambia MTANZANIA kuwa kwa muda wa miezi miwili ilibanika kushuka kwa kasi kwa mapato Kituo cha Kimara kutoka makusanyo ya Sh milioni 20 hadi 25 kwa siku wakati yaliyokuwa yakikisanywa kupitia mfumo wa kieletroniki na kufikia hadi Sh milioni 10 kwa siku.

Hatua hiyo iliifanya Serikali kupitia Wakala wa  Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART), kufanya uchunguzi wa kina na kubaini mtandao huo wa wizi huku mmoja wa kigogo wa juu wa Kampuni ya Uda-Rapid Transit (UDART), naye akishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na mtandao huo.

Inadaiwa wafanyakazi hao kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa (majina yanahifadhiwa kwa sasa kwa sababu za kiuchunguzi),  waliunda mtandao maalumu wa kufyatua tiketi feki na kujipatia mamilioni ya fedha.

Mradi huo wakati unaanza mwaka 2016, ulikuwa unabeba abiria 75,000 na kwa sasa idadi hiyo imeongezeka hadi kufikia 200,000 na  kwa kila safari hulazimika kulipa Sh 650 ukijumlisha kwa idadi hiyo mapato kwa siku yaliyokuwa yanakusanywa hufikia Sh milioni 130,000 ingawa kwa sasa yameshuka.

Katika mtandao huo imebainika mbali ya kufyatua tiketi feki pia wamekuwa wakifanya ujanja kwa kuwauzia watu wazima tiketi za wanafunzi ya Sh 200 badala ya Sh 650 huku kiwango kinachobaki kikingia katika mifuko ya wajanja.

Hatua hiyo ilieleta mshtukio na kupelekea kuundwa kwa timu ya siri kwa ajili ya kuchunguza mtandao huo ambapo timu hiyo iliundwa na maofisa kutoka Wakala wa Mabasi ya Yaendayo Haraka (DART), Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya dola ambapo walibaini mtandao huo ulijinufaisha kwa zaidi ya miezi miwili kwa kuvuna mamilioni.

MTANZANIA ilipomfuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alithibitisha kukamatwa kwa maofisa hao ambao bado wanaendelea na uchunguzi nao.

“Ni kweli tumewakamata (Ijumaa) na tunaendelea kuwakamata mtandao mzima ili tujue kwa kina namna wanavyoikosesha serikali mapato yake. Ule mradi ni wa serikali ni lazima ulindwe kila aliyetafuna kila senti kinyume cha sheria tutamfikia ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

“Wengi tuliowakamata wengi ni wakusanya fedha katika vituo na si hao tu sasa tunakwenda kuvunja mtandao mzima wa wizi huu wa fedha za umma. Fedha ni lazima ikusanywe kwa utaratibu ili serikali ipate mapato yake na si vinginevyo,” alisema Kamanda Mambosasa

KAULI YA DART

MTANZANIA ilimtafuta Mtendaji Mkuu wa DART, Mhandisi Ronald Lwakatare, ambaye alithibisha kukamatwa kwa wafanyakazi hao.

“Kulikuwa na jitihada za kukamatwa watu ambao wanaohusika na upotevu wa mapato na zoezi hili tulilonalo  ni endelevu wakati tunaendelea na kazi ya kusimamia mradi huu pia ni wajibu wetu kusimamia mapato.

“Zoezi hili hufanyika mara kwa mara na wafanyakazi wanaokamatwa huchukulia hatua husika. Kwa watu hufanya ujanja tu katika kufanyakazi za ukeshia hapo (vituo). kuna tatizo la kuuza tiketi za wanafunzi kwa watu wazima na kadhalika.

“Ni mchezo ambao hunafanywa sana lakini ukiangalia kwa upana wake kama linafanyika kwa muda mrefu huleta mpotevu mkubwa wa fedha. Na hili huchangiwa kwa kutokuwa na wafanyakazi ambao ni waaminifu,” alisema Lwakatare

MBIA WA PILI

Alipoulizwa mchakato wa kumpa mbia wa pili kwa ajili ya kuendeshaji wa mradi huo wa mabasi ya mwendokasi, Lwakatare, alisema bado na mchakato huo ambao awali ulikwenda lakini hawakuweza kuhitimisha.

“Masuala ya manunuzi kwa hiyo tupo mbioni kutafuta mtu atakayeleta huduma ya mabasi na tunaendelea na juhudi za kumpata na tunaamini tutafika mwisho. tunajitahidi sana kuhakikisha kuna mabasi ya kutosha kwa sababu mwitikio umekuwa mkubwa sana,” alisema

UJENZI NJIA YA MBAGALA

Mtendaji Mkuu huyo wa DART, alisema kwamba kwa sasa wapo mbioni kukamilisha taratibu wa mkandarasi wa ujenzi wa njia ya mradi wa Mbagala ambapo wakati wowote ataanza kazi mwishoni mwa mwaka huu.

BARABARA YA JUU UBUNGO

Alisema changamoto iliyopo sasa ni ujenzi wa Fly over Ubungo hasa katika Kituo cha Ubungo Maji kwa sasa watafanya mabadiliko ya kituo hicho kutokana na ujenzi huo na sasa wako mbioni kubadili kituo hicho.

“Ujenzi was Fly Over ya Ubungo, hasa katika eneo letu la Ubungo Maji sasa tunajitahidi kuhakikisha tunabadili kituo kingine ili watu wawe salama. Tunaelewa ni kituo kinachopendwa na watu wengi nasi kama Dart siku zote tunajali usalama wa watu,” alisema

MCHEZO ULIPOANZA

Aprili 24 na Mei 16, mwaka huu makusanyo za yaanza kuhujumiwa baada ya UDART kuingilia kati na kurtaka kukusanya wao fedha huku wakipinga uwepo wa tiketi za Kiletroniki chini ya Kampuni ya Maxcom Afrika Plc.

Hatua hiyo iliifanya UDART kuingilia na kusimamia ukusanyaji wa mapato kupitia tiketi maalumu za mashine huku zikichanwa na wafanyakazi waliowekwa milango.

Awali mradi huo ulipoanza suala la makusanyo lilikuwa chini ya Kampuni ya Maxcom Africa ambao walikuwa wakikusanya Kieletroniki na udhibiti wa wizi huku UDART wakibaki na uendeshaji mabasi.

Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka kwa sasa unaendeshwa kwa ubia na Kampuni ya Uda-Rapid Transit (UDART ), huku mbia mkubwa akiwa Kampuni ya Simon Group katika awamu ya kwanza ya majariobi ya mradi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles