27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mayanja: Tutafika uwanjani tukijiamini

mayanja.*Ninaamini hakuna aliyefanikiwa kusoma mbinu zetu

NA SAADA SALIM, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja, amesema amefurahishwa na sehemu waliyoweka kambi kwani hakuna mpinzani wao yeyote aliyefanikiwa kuzijua wala kusoma mbinu zake za kuwamaliza watani wao wa jadi Yanga, hali inayowafanya kufika uwanjani kesho wakijiamini.

Simba imeweka kambi katika Chuo cha Biblia mjini Morogoro, kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mayanja alisema muda wote waliokaa katika kambi hiyo hakuna aliyefanikiwa kuzisoma mbinu zao, hali iliyomfanya atambe kupata ushindi katika mchezo wao huo.

Alisema mandalizi yake yanaendelea vizuri na tayari ameshatoa majukumu kwa vijana wake, katika kuhakikisha wanawachapa wapinzani wao hao.

“Naifahamu vizuri sana Yanga, hivyo nimewaandaa vijana wangu hasa safu ya ushambuliaji jinsi ya kutumia nafasi nzuri ya kupata mabao, nikiamini hakuna mtu aliyefanikiwa kuzisoma mbinu zetu,” alisema.

Mayanja alisema hawezi kuzitaja hadharani mbinu zake alizowapa wachezaji wake, wataziona siku ya mchezo akiamini kwamba ni kipimo cha kukijenga kikosi chake.

“Hii mechi ni kipimo kwangu kwa mashabiki kuona uwezo wangu, hivyo tayari nimeshatoa majukumu kwa wachezaji wangu, sasa kazi kwao kuhakikisha wanapata ushindi,” alisema.

Mayanja alisema kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo, Yanga anaichukulia kama timu nyingine hivyo ana matumaini makubwa na wachezaji wake kutomuangusha katika mchezo huo.

Simba ilitarajiwa kurudi Dar es Salaam jana usiku tayari kwa mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu, wakifika watakutana na viongozi mbalimbali wa timu kabla ya mchezo huo. Pia baadhi ya matawi yamejipanga kuchangisha fedha ili kuwapa wachezaji kama motisha wakishinda.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles