27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mayanja ‘awachana’ wachezaji Simba

mayanja-akiwa-kazini-simba_1836bf5vzqefk17bhy3wmcr520NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Jackson Mayanja, amesema kitendo cha baadhi ya wachezaji kujihusisha na mambo yasiyowahusu nje ya uwanja kimechangia kufanya vibaya na kuondoshwa kwenye michuano ya Kombe la FA.

Ndoto za Simba kucheza Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani, ziliyeyuka juzi baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kocha huyo raia wa Uganda amewatupia lawama wachezaji wake, akidai kuwa baadhi yao wanashinda kutwa nzima kwenye mitandao ya kijamii wakifanya mambo yaliyo nje ya utaratibu wa taaluma yao na kusababisha matatizo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mayanja alisema hali hiyo inawafanya washindwe kutimiza majukumu yao uwanjani, kwani inafika wakati anampanga mchezaji akitarajia atafanya vizuri lakini matokeo yake wanamwangusha.

“Wachezaji kama hawazingatii maadili ni vigumu timu kufanya vizuri, ndio maana jana (juzi) hatukufanya vyema kutokana na wengine kuwa majeruhi na baadhi kuchelewa mazoezi huku wakiomba ruhusa bila mpangilio,” alisema.

Mayanja aliwataja wachezaji Hamis Kiiza na Jjuuko Murshid kuwa ni miongoni mwa waliochangia kupata matokeo mabaya, kutokana na kuchelewa  kujiunga mazoezini kwa wakati.

Hata hivyo, kocha huyo alisema matokeo hayo si kipimo cha wao kufanya vibaya katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, bali yataongeza hamasa ya kufanya vizuri zaidi.

Kwa kipigo cha juzi, Wekundu hao wa Msimbazi wameshindwa kuungana na mahasimu wao Yanga, Azam FC na Mwadui waliotangulia hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles