27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

May, Merkel kukutana Berlin

Berlin, Ujerumani

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, atakutana na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, Berlin, leo kwa mazungumzo kuhusu Brexit, siku moja baada ya zoezi la kuyapigia kura makubaliano ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya kuahirishwa.

May ameahirisha zoezi hilo baada ya kugundua makubaliano hayo yangepingwa bungeni kwa sasa anajaribu kuwatanabahisha viongozi wenzake wa Umoja wa Ulaya, na wale wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya, waridhie makubaliano hayo yafanyiwe marekebisho.

Wawakilishi wa Ujerumani na Ufaransa, pamoja na mwenyekiti wa baraza la Ulaya, Donald Tusk, wanapinga kujadiliwa upya makubaliano hayo.

Hata hivyo, Tusk amepanga kuzungumza na May, Alhamisi wiki iliyopita viongozi wa Umoja wa Ulaya watakapokutana mjini Brussels.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya ameondoa uwezekano wa kujadiliwa upya makubaliano ya Brexit.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles