MAULID MTULIA: “NASUBIRI KUAPISHWA KUWA MBUNGE WA KINONDONI”

Na Asha Bani –


Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Maulid Mtulia amesema anasubiri kuapishwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kutokana na mgombea aliyepitishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa mwepesi kwake.

Kamati Kuu ya Chadema jana imemteua Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu kuwa mgombea wa Jimbo la kinondoni kupambana na Mtulia.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Jumamosi Januari 20, Mtulia ambaye anarudisha fomu yake leo mchana amesema tayari ameshashinda mapema na kwamba anasubiri kuapishwa.

Awali, Mtulia alikuwa Mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kabla ya kukihama chama hicho kwa madai ya kumuunga mkono Rais John Magufuli katika utendaji wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here