25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Matukio ya ukatili wa jinsia 1,437 yaripotiwa Arusha

ELIYA MBONEA, ARUSHA

Mkoa wa Arusha umetajwa kuwa na matukio 1,437 ya ukatili wa jinsia kwa wanawake na watoto katika kipindi cha mwaka 2017 mpaka 2018.

Matukio hayo na yasiyoripotiwa maeneo maalum yanaufanya mkoa huo kuwa wa tatu kitaifa kwa kuwa asilimia na 41, chini ya Dodoma asilimia 47 na Manyara asilimia 58.

Hayo yamebainishwa leo Juni 11, na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega alipokuwa akifunga mafunzo ya wanahabari kuhusu umuhimu wa nafasi ya vyombo vya habari kutetea afya na maendeleo ya vijana.

Mafunzo hayo yameratibiwa  na Shirika  linalojishughukisha na masuala ya vijana la Deutsche Stiftung Weltbevolkerung (DSW) ofisi ya Tanzania.

Alisema kundi la wanahabari linalojukumu kubwa la kutafuta, kuandika, kutangaza matukio ya habari za ukatili ndani ya jamii.

“Wanahabari ndio kiunganishi cha ukelezaji wa masuala ya maendeleo, afya na ukatili wa kijinsia,” alimesema Kwitega.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa DSW Tanzania, Peter Sanga, amesema mipango waliyonayo kama shirika imelenga kuchangia vipaumbele vya mkoa wa Arusha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles