27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mattaka wa ATCL akaangwa Kortini

David Mattaka
David Mattaka

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

UPANDE wa Jamhuri umedai mahakamani kwamba aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka, alisaini mkataba wa kukodisha ndege iliyokuwa katika matengenezo na kusababisha Serikali kupata hasara zaidi ya Sh bilioni 71.

Hayo yalibainika jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Respicious Mwijage, wakati Jamhuri walipokuwa wakiwasomea washtakiwa maelezo ya awali ya kesi inayowakabili.

Mbali na Mattaka, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ambao walisomewa maelezo ya awali jana ni vigogo kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), ambao ni Ofisa Mtendaji Mkuu mstaafu, Dk. Ramadhan Mlinga na Mwanasheria Bertha Soka.

Wakili wa Serikali Mkuu, Timon Vitalis, kwa kushirikiana na Wakili wa Serikali, Timon Peter, waliwasomea washtakiwa hao maelezo ya awali mbele ya Hakimu Mwijage.

Wakili Vitalis alidai kesi hiyo inahusu ukodishaji wa ndege A 320-214 na kwamba mkabata uliingiwa kati ya Wallis Trading Inc ya Liberia na ATCL.

Alidai mkataba ulisainiwa Oktoba 9, 2007 na Mattaka alisaini kwa niaba ya ATCL na Andrew Wettern kwa niaba ya Wallis Trading Inc.

“Novemba, 2002 Serikali iliuza asilimia 51 ya hisa zake za Shirika la Ndege (ATC) kwa Shirika la Ndege la Afrika Kusini na katika kipindi hicho ATC ikawa kampuni binafsi na jina lake likabadilika kutoka ATC na kuwa ATCL.

“ATCL ilisajiliwa chini ya sheria za kampuni ambapo Serikali ilikuwa mmiliki na mkataba kati ya Serikali na Shirika la Ndege la Afrika Kusini ulifikia kikomo mwaka 2006 ambapo Serikali iliichukua ATCL.

“Machi 13, 2007 Kampuni ya China iitwayo China Sanangol International Holding Limited (CSIHL) ilitambulishwa kwa menejimenti ya ATCL kama wawekezaji wapya ambao wanataka kuwekeza kwenye kampuni hiyo,” alidai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles