29.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya umeya Kinondoni yapangiwa hakimu

jaji-mkuu-wa-tanzania-mohammed-chande-othman
Jaji Mkuu, Othman Chande

 

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

KESI ya kuomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itengue matokeo ya umeya na unaibu meya katika Manispaa ya Kinondoni na iamuru uchaguzi urudiwe, imepangwa kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage.

Ilifunguliwa juzi katika mahakama hiyo na jana ilisajiliwa na kupewa namba 304/2-16 na kupangiwa hakimu wa kuisikiliza.

Wadai katika kesi hiyo ni aliyekuwa mgombea umeya, Mustafa Muro na naibu wake, Jumanne Mbunju, ambao wanawakilishwa na Wakili John Mallya.

Wakili Mallya akiwakilisha wateja wake, alifungua kesi dhidi ya walioshinda nafasi hizo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Meya Benjamin Sitta na Naibu Meya Manyama Mangaru, Ofisa Utawala wa Manispaa hiyo na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao kilichowachagua viongozi hao.

Kwa mujibu wa madai waliyowasilisha mahakamani, wadai wanaiomba mahakama hiyo pamoja na mambo mengine itengue matokeo ya uchaguzi huo, iamuru urudiwe na Mkurugenzi wa Manispaa afuate taratibu na kanuni.

Wanadai walifungua kesi hiyo kupinga kikao hicho ambacho kilikuwa kikao maalumu kwa kuwa walalamikiwa walikaa wao wenyewe, kuchanguana kwa kufuata taratibu na kanuni za kwao wenyewe.

Muro ambaye ni Diwani wa Kinondoni kupitia Chadema, alidai kikao hicho hakikufuata taratibu na kanuni zilizoko, badala yake watu walikaa na kuamua kuchaguana kwa ajili ya mambo yao.

Kwa upande wake, aliyekuwa mgombea Naibu Meya, Mbunju, alidai wameamua kufika mahakamani kwa ajili ya kutafuta haki kwa sababu wanaamini kuna taratibu zimekiukwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles