25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

‘MATEJA’ WAGEUKIA UJASIRIAMALI

 

WATUMIAJI wa dawa za kulevya wanaopelekwa kwenye  Hospitali ya afya ya akili na utengamao ya Lutindi iliyopo wilayani Korogwe mkoani Tanga, wamegeuka kuwa mafundi baada ya kufundishwa namna ya kutengeneza samani na kapeti.

Vitu ambavyo wamekuwa wakivitengeneza ni viti vya

majumbani, hotelini, kapeti za chini ya miguu na vitu ambavyo

vinatumiwa na wananchi katika matumizi yao, jambo ambalo linawafanya kujiandaa na kujiajiri wakati wanapomaliza matibabu yao.

 

Akizungumza jana, Muuguzi Msaidizi wa Hospitali hiyo, Amina Ramadhani, alisema baada ya kuwapokea wagonjwa hao wanakaa nao kwa kipindi fulani na watakapokuwa wamepata nafuu watawafundisha namna ya kujifunza ufundi wa kutengeneza samani.

Alisema miongoni mwa vitu ambavyo wamekuwa wakifundishwa ni kutengeneza bidhaa hizo ambazo soko lao kubwa lipo kwenye wilaya za Bagamoyo, ikiwamo maeneo mengine ndani ya Tanzania.

“Unajua tunapowapokea wagonjwa hawa sisi kama hospitali baada ya kuona wamepata nafuu kidogo, tunaamua kuwaingiza kwenye suala la ufundi seremala ambapo asilimia kubwa wamekuwa wakifanya vizuri badala ya kukaa bila kufanya kazi,” alisema.

“Lakini tunaweza kusema hili ni moja kati ya mafanikio yetu makubwa kwani mgonjwa anapokuja kwenye hospitali hii mara nyingi unakuta anashinda wodini tu, lakini anapopata nafuu basi wanaingia kwenye mambo ya ufundi,” alisema.

Alisema sababu kubwa ya kuingia kwenye shughuli za ufundi wanapokuwa huko ni kuwaandaa wakati wanapopona na kwenda kwenye jamii waweze kujiajiri kutokana na ujuzi ambao wanakuwa wameupata.

Alisema wagonjwa hao wanapokuwa wakifundiswha masuala ya ufundi inawasaidia kuondokana na utegemezi mara baada ya kupona  ambao hurudishwa walipotoka.

Akizungumza mmoja wa wagonjwa wanaohudumiwa na hospitali hiyo, Abdi Mohamed ambaye alitoka Wilaya ya Kigamboni, Dar es Salaam alisema suala la kufundishwa ufundi wa kutengeneza vitu mbalimbali limewapa mwanga wa kijiajiri.

“Kwa kweli hii ni fursa nzuri kwetu kwani si kwamba inatujenga bali pia kutuandaa  kuona namna bora ya kujiajiri wakati tunapotoka hapa baada ya kupona.

“Lakini pia niwaase vijana wenzangu kuachana na matumizi ya dawa za kulevya kwa sababu si mzuri na yameharibu maisha ya watu wengi kwenye jamii wanazotoka,” alisema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles