28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Masheikh waja juu Mahakama ya Kadhi

5Na WAANDISHI WETU
VIONGOZI wa dini ya Kiislamu wamepinga tamko lililotolewa na Jukwaa la Wakristo kuhusu sheria hiyo ya kuanzishwa Mahakama ya Kadhi na kudai kuwa matamko ya aina hiyo yanaweza kusababisha machafuko nchini.
Kauli hiyo zimekuja siku moja baada ya Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) kutoa waraka, likipinga muswada unaopendekeza kuanzishwa Mahakama ya Kadhi unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni wakati wowote.

Akizungumza na MTANZANIA Imamu wa Msikiti wa Idrisa uliopo Kariakoo, jijini Dar es Salaam, Sheikh Ally Basalehe alisema viongozi wa dini ya Kikristo mara nyingi wamekuwa wakipinga masuala mbalimbali yanayogusa Uislamu yakiwamo yale mazuri.
Alisema mwenendo wa kupinga masuala ya kidini sio mzuri, kwani Waislamu hawajatamka kuwa sheria za dini hiyo zitawale nchini isipokuwa mahakama hiyo itajali masuala muhimu yakiwamo ya ndoa na mirathi.
Kwa upande wake Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Rajabu Katimba, aliiambia MTANZANIA kwa njia ya simu jana kuwa kwa Waislamu Mahakama ya Kadhi ni ibada kama ibada nyingine, na haipaswi kupingwa na chombo kingine cha dini kutokana na umuhimu wake.
“Tunawashangaa viongozi wa dini ya Kikristo kusema suala hili ni la kibaguzi, mbona Serikali imeingia mkataba na hospitali za makanisa mwaka 1992 na wanapewa mabilioni ya fedha za kodi za Watanzania wakiwamo Waislamu sisi hatujawahi kuhoji wala kulalamika?” alihoji Sheikh Katimba.
AG awatoa hofu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, amewatoa hofu Wakristo wanaohofia mpango wa Serikali wa kuitambua kisheria Mahakama ya Kadhi nchini.

Alisema pamoja na kwamba mpango huo umeanza kulalamikiwa na baadhi ya makundi ya kidini, nia hiyo haina madhara kwa wananchi kwa kuwa Serikali haiwezi kupitisha sheria itakayowagawa watu.

AG Masaju alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Bunge.

“Napenda kuwaambia kwamba hakuna sheria inayotungwa na kukubalika moja kwa moja. Kwahiyo, sheria inapotungwa na Bunge, kamati husika za Bunge zinashirikishwa, na wananchi kwa upande wao wanashirikishwa ili watoe maoni yao juu ya sheria hiyo,” alisema AG Masaju.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles