24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Masheikh sita waliotekwa DRC waachiwa

LiberataNA ASIFIWE GEORGE, DAR ES SALAAM

MASHEIKH sita wa Tanzania waliochukuliwa mateka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wameachiwa huru usiku wa kuamkia jana.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Liberata Mulamula, alisema Balozi wa Tanzania nchini DRC kwa sasa yupo njiani kuelekea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Goma kwa ajili ya kuwaona mateka hao.

Alisema taarifa za kutekwa watu hao zilitolewa mwanzoni mwa Agosti mwaka huu ambapo Serikali ilifanya juhudi ya kufuatilia na kufanya uchunguzi juu ya taarifa hizo.

Mulamula alisema  inasemekena watu hao wa taasisi ya kuhubiri dini ya Kiislamu walitekwa na kikundi cha waasi ambapo hadi sasa hakijajulikana.

Alisema watekaji wao walidai wapewe kiasi cha dola za Marekani 40,000 (sawa na Sh milioni 128.7 ) ili wawaachie Watanzania hao huru ambapo waliwaomba kupunguziwa hadi kufikia dola 20,000.

“Nchi yetu haijawahi kutokea kukamatwa mateka, lakini tunaipongeza Serikali ya DRC kulifuatilia hili na kutupatia taarifa,” alisema Mulamula.

Aliwataka wananchi wanaokwenda nchi za ugenini kutoa taarifa katika ubalozi au Wizara ya Mambo ya Ndani ili waweze kutambua haraka linapotokea tatizo kama hilo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya nje Zanzibar, Silima Kombo Haji, alisema watekaji hao walitumia ujanja wa kupiga simu kwa ndugu zao pamoja na watu wa karibu na Kijiji cha Goma.

Alisema juzi watekaji hao walikuwa wakipiga simu wakisisitiza kuwa muda umekwisha, hivyo fedha hizo zipelekwe haraka kabla hawajawadhuru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles