30.8 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

MASHABIKI SIMBA WAITWA MBEYA

WINFRIDA MTOI

KOCHA Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo na Tanzania Prisons kushudia Mnyama akiandika historia ya kuchukua ubingwa mara ya tatu mfululizo.

Simba ambayo juzi iliichapa Mbeya City mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, watakaotumia tena Jumapili hii.

Mchezo na Prisons endapo Wekundu wa Msimbazi hao watafanikiwa kushinda, hakuna wa kuwazuia kujiita mabingwa wa msimu 2019/2020.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Wanamsimbazi hao wanaongoza  na pointi 78 na zimebaki alama mbili pekee kutangazwa mabingwa baada ya Yanga na Azam kushindwa kuchukua pointi tatu  juzi katika michezo yao.

Akizungumza na baada ya mchezo na Mbeya City ulikusanya watu mbalimbali, Matola, alisema anatarajia kuona Wanasimba walijaza dimba la Sokoine Jumapili zaidi ya walivyojitokeza juzi.

Alisema amefurahishwa na muitikio wa wapenzi hao wa Simba, kwani ndiyo ilikuwa chachu ya ushindi wa waliopata kwa Mbeya City.

“Niwapongeze Wanasimba waliojitokeza wengi kuwapa sapoti, ninachowaambia hatutawaangusha tutafanya kile wanachotamani sisi kukifanya, naomba waje tena kwa wingi kutupa sapoti,” alisema Matola.

Akizungumzia mchezo na Mbeya City, alisema wachezaji walifanya kitu walichowaelekeza muda mfupi kabla ya mchezo kutokana na hali waliyokutana nayo Mbeya.

“Wachezaji wameweza kufanya kile tulichowatuma, imekuwa ni ngumu kwetu kutokana na uwanja haukua mzuri na kutufanya kucheza mpira ambao hatujauzoea, lakini niwapongeze wachezaji wamepambana,” alisema.

Naye nahodha wa kikosi hicho, John Bocco ambaye ndiye mfungaji wa mabao hayo, alisema siri kubwa ya kile wanachokifanya ni ushirikiano na umoja waliokuwa nao wachezaji.

“Tumejitolea kila mchezaji kupata ushindi huu, ninachofurahia tunacheza kwa ushirikiano mkubwa na kutufanya tuwe na kiwango cha kizuri, tunaelekeza nguvu zetu mchezo ujao,” alisema Bocco.

Mshambuliaji huyo alisema hawatajibweteka na ushindi huo, wamejipanga kucheza kila mechi kwa kujituma hadi dakika ya mwisho watakayokabidhiwa ubingwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles