Na CHRISTOPHER MSEKENA
BAADA ya kufanya vyema na wimbo, Cheza aliomshirikisha Enock Bella, msanii wa kizazi kipya anayeshi nchini Canada, Maombi M’meba a.k.a Marhox, amerudi kivingine na cover ya Jérusalema kutoka kwa Master KG wa Afrika Kusini.
Tangu enzi za utoto wake, Marhox amekuwa akiimba kwenye kwaya tofauti na kufanya uimbaji na uandishi wa mitindo ya muziki kama vile RnB, Zouk, AfroPop na nyingine kibao.
Akizungumza hivi karibuni, Marhox ambaye nyimbo zake zimekuwa zikigusa maisha, upendo na kueleza upinzani wake dhidi ya ukatili wa vita na udhalimu unaofanyika kwenye nchi yake ya asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.
“Nimeachia cover ya Jerusalem ambayo nimeiimba kwa Kiswahili, naamini mashabiki zangu watafurahia kwasababu ni ngoma nzuri pia inapatikana kwenye chaneli yangu ya YouTube ikiambatana na albamu yangu ya pili unayoweza kuipata kwenye mitandao ya iTunes, Spotify, Amazon, Google Play nk,” alisema Marhox.