Addis Ababa, Ethiopia
Nchi ya Marekani imetangaza kuweka vikwazo vya kiuchumi na usaidizi wa kiusalama dhidi ya nchi ya Ethiopia kufuatiwa machafuko katika mji wa Tigray.
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, pia ametangaza marufuku ya usafiri dhidi ya maafisa wa Ethiopia na Eritreano pamoja na wengine ambapo wanatuhumiwa kufanya ukatili.
Waziri Blinken amesisitiza kuwa hatua ya kimataifa inahitajika ili kusaidia katika utatuzi wa mzozo huo na kuongeza kuwa wale waliopewa dhamana hawajachukua hatua madhubuti kukomesha uhasama.
Maelfu ya watu wameuawa na wengine kadhaa kuachwa bila makao tangu mzozo ulipozuka miezi sita iliyopita huku pande zote mbili zimelaumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.
Mapema siku ya Jumapili serikali ya Ethiopia ilipuuzilia mbali madai ya raia katika eneo la Tigray lililokumbwa na vita walilengwa kwa silaha za kemikali kutoka kwa majeshi ya Ethiopia au Eritrea.