33.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani kumpeleka mwanamke wa kwanza mwezini 2024

WASHINGTON, MAREAKANI 

SHIRIKA la anga la Marekani (Nasa) limetangaza rasmi mpango wake wa kurejea tena mwezini utakaogharimu dola bilioni 28 ifikapo mwaka 2024.

Kama sehemu ya mpango unaojulikana kama Artemis, Nasa itawapeleka mwanaume na mwanamke mwezini kwa mara ya kwanza tangu binadamu kufika huko mwaka 1972.

Lakini mpango huo utategemea na iwapo Bunge la Marekani litaidhinisha jumla ya dola bilioni 3.2 za kununua vifaa vitakavyotumiwa katika safari hiyo.

Wanaanga watasafiri kwenye chombo kilicho na muundo wa maalum kinachofahamika kama Orion na ambacho kitarushwa angani kupitia roketi itakayotumia mfumo unayojulikana kama SLS.

Akizungumza mwezi Septemba, 21 msimamizi wa Nasa Jim Bridenstine alisema: “Dola bilioni 28 zitatumiwa kugharamia shughuli zitakazohusiana na safari hiyo katika kipindi cha miaka minne kufadhili mpango wa Artemis kwenda mwezini.

Ufadhili wa SLS, ufadhili wa Orion, binadamu watakaotumia chombo hicho kwenda mwezini – vyote hivyo ni vitu vitakavyokuwa vimejumuishwa kwenye mpango wa Artemis .”

Lakini alifafanua kuwa: “Bajeti iliyowasilishwa mbele ya mikutano yote miwili ya bunge kwa sasa inajumuisha dola bilioni 3.2 ya mwaka 2021 itagharamia mfumo utakawapeleka binadamu mwezini, ni muhimu sana tupate fedha hizo, dola bilioni hizo 3.2.”

Bunge la Wawakilishi nchini Marekani limepitisha mswada wa kulipatia shirika hilo dola milioni 600 kwenda mwezini.

Lakini Nasa inahitaji fedha zaidi kutengeza chombo kamili kitakachotumika kwa safari hiyo.

Bridenstine aliongeza kusema: “Kwamba tunalishukuru sana Bunge kwa hatua hiyo, lakini tumetathmini bajeti yetu tukaonelea umuhimu wa kufadhili mfumo utakaotumiwa na binadamu – na hizo dola milioni 600 zitatumika katika mchakato huo. Pia ni keeling tunaomba kupewa dola bilioni 3.2 kwa jumla.”

Mwezi Julai mwaka 2019 Bridenstine aliambia kitengo cha habari cha CNN kwamba mwanamke wa kwanza atazuru mwezini mwaka 2024 na atakuwa “mtu atakayethibitishwa, mtu aliyesafiri, mtu ambaye tayari atakuwa amefika katika kituo cha kimataifa cha angani”.

Pia alisema atakuwa mtu ambaye tayari ni mtaalamu wa anga za mbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles