Mwandishi Wetu
TAASISI ya Dk Reginald Mengi Kwa Watu Wenye Ulemavu (DRMF) imetangaza utaratibu wa kumuenzi Dk Mengi kwa mwezi mzima, kupitia shughuli mbalimbali zitakazofanyika katika mwezi wa Mei 2020.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Shimimana Ntuyabaliwe, alisema mwezi wa Mei ni muhimu kwao kwa sababu umebeba matukio matatu muhimu ambayo ni kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu muasisi wa DRMF alipofariki Mei 2, 2019, pia siku yake ya kuzaliwa ni Mei 29 na Mei 18 2018 taasisi hiyo ndipo iliposajiliwa rasmi.
“Kwa hiyo, katika mwezi huo tutaendesha kampeni ya kuwahamasisha Watanzania popote pale walipo, taasisi, mashirika, na vikundi vya kijamii kuutumia mwezi wa Mei kila mwaka kufanya matendo mbalimbali ya kujitolea kwa kumbukumbu ya Dk. Reginald Mengi. Kampeni hii itajulikana kwa jina la Ubuntu.
“Ubuntu ni neno la kabila la wazulu kutoka Afrika ya Kusini likimaanisha ‘Utu’ au ‘Moyo wa kujitolea kwa binadamu wenzako’ hivyo taasisi yetu inaamini kuwa neno hili moja Ubuntu linatosha kumtambulisha marehemu Dk. Mengi kikamilifu,” alisema Ntuyabaliwe.
Aliseam katika uhai wake Dk. Mengi alijitolea na kufanya mambo mengi katika jamii ya watanzania n mkono wake ulikuwa mrefu na mpana na alijitoa akiwa na tabasamu la bashasha bila kuchoka, kwa kugusa na kuleta tofauti katika maisha ya Watanzania wengi aliowafikia.
“T