28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Ujenzi: Mvua zitanyesha hadi Aprili

Ramadhan Hassan -Dodoma

WIZARA ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, imesema  mvua zitaendelea kunyesha nchini mpaka Aprili, mwaka huu, hivyo kuwataka Watanzania kuzidi kuchukua tahadhari na kufuata ushauri wa wataalamu.

Hayo yalielezwa juzi na Waziri wa Wizara hiyo,Isack Kamwelwe alipozungumza na waandishi wa habari ofisini jijini Dodoma.

Alisema mwaka huu, Tanzania imepokea mvua nyingi zisizo za kawaida ambazo zilianza tangu Oktoba na kuunganisha na msimu wa masika.

Alisema mvua hizo, ni matokeo ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tanianchi ambapo alidai hali hiyo imesababisha kuwapo kuongezeka la joto la bahari juu ya wastani kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi.

Alisema mpaka sasa mvua zimenyesha kwa kiwango cha juu ya wastani katika maeneo mengi ambapo Dodoma ilinyesha kwa milimita 471.1 sawa na asilimia 127 juu ya wastani wa milimita 369.5.

Alisema mkoani Iringa,ilinyesha milimita 782.2 sawa na asilimia 210 juu ya wastani wa milimita 371.9,Sumbawanga milimita 520.8 sawa na asilimia 215 juu ya wastani wa milimita 462.2.

“Pamoja na viwango hivi kuwa juu ya wastani, maeneo bado mvua zinatarajiwa kuendelea kunyesha mpaka Aprili,mwaka huu zitakapopungua,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles