24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

Maonyesho ya Picha kuhusu mabadiliko ya tabianchi yazinduliwa Dar

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Ubalozi wa Ufalme wa Uholanzi nchini Tanzania umefanya ufunguzi wa wa sherehe za kipekee za monyesho ya picha za Mabadiliko ya Tabianchi.

Balozi wa Ufalme wa Uholanzi nchini, Wiebe de Boer, akizungumza wakati wa ufunguzi huo.

Akizungumza leo Jumanne Februari 8, 2022, Balozi wa Ufalme wa Uholanzi nchini, Wiebe de Boer amesema lengo la kuandaa maonyesho na matukio hayo ni kuongeza uelewa nchini juu ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Ni matarajoo yetu kuwa maonyesho haya yatahamasisha watiu hasa vijana kuchukua hatua kwa pamoja dhidi ya mabadiliko haya.

“Hivyo maonyesha haya yataonyesha hadithi mbalimbali za picha zenye athari kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa toka kwa wapiga picha nane wa Tanzania na Kenya.

“Aidha, yanalenga kuongeza uelewa wa mabadiloko ya tabianchi katika nchi za Afrika Mashariki kwani kama tunavyofahamu kwamba kazi za upigaji picha zinaonyesha mtazamo wa kila mpiga picha juu ya changamoto ya hali ya hewa zinazosababishwa na athari za shughuli za kila siku zinazofanywa na wenyeji hadi kuathiri ulimwengu kwa ujumla,” amesema Balozi Boer.

Picha hizo pia zitaonyeshwa pamoja na kazi za mwanahabari wa kimataifa wa Uholanzi, Kadir van Lohuizen, ambaye ni mshindi wa tuzo kupitia mradi wake wa muda mrefu kuhusu changamoto za hali ya hewa unaofahamika kama ‘After Us the Deluge‘ yaani Baada yetu ni Mafuriko.

“Natumai kwamba mradi wa Baada yetu ni Mafuriko utachangia ufahamu bora wa kile kinachotokea hii leo na itatusaidia sisi wote kutambua kwamba hatuna wakati wa kupoteza katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi” amesema Lohuizen.

Mmoja wa wapiga picha hao, Michael Mbwambo kutoka Tanzania ambaye alipata shule kutoka NOOR pamoja na Ubalozi wa Uholanzi kuhusu mabadiliko ya tabianchi amesema kuwa kupitia kazi zao wanazopzifanya ambazo ni kupiga picha wanauwezo wa kuelimisha jamiii hususan kizazi cha sasa kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

“Kwa elimu hii tuliyoipata ni kwamba sisi kama Watanzania hatuhitaji kusubiri mtu kutoka nje ndio aje atueleze kuwa mazingira haya ndio mabadiliko ya tabianchi jambo ambalo sasa tutalifanya wenyewe.

“Hivyo elimu hiyo tuliyoipata ilikuwa ni bora zaidi kwetu Watanzania na tutatumia ujuzi huo kuhamasisha kulinda mazingira yetu kwa ajili ya maisha yetu ya baadate,” amesema Mbwambo.

Aidha, sambamba na maonyesho hayo, Ubalozi wa Uholanzi umeandaa Mazungumzo ya tabianchi mawili ambayo yanalenga kuchochea uhamasishaji kuhusu hatua za hali ya hewa yatakayofanyika Februari 10 na 24.

“Februari 10 kutakuwa na mazungumzo ya hali ya hewa kuhusu kujenga mifumo ya chakula inayostahimili hali ya hewa Tanzania na Februari 24, kutakuwa na majadiliano ya hali ya hewa kuhusu ‘Kuchukua hatua juu ya maisha yetu yajayo’ambayo yanalenga zaidi vijana ambao ni kizazi cha kesho na nafasi yao katika kuchukua hatua dhidi ya hali ya hewa. Aidha, siku ya Ijumaa Februari 11, Lohuizen atatoa somo kuhusu madhara ya kibinadamu yas kupanda kwa kina cha bahari,”.

Jumatano ya Februari 3, 2022 ndiyo maonyesho haya yatafunguliwa rasmi hadi Machi 3, mwaka huu Alliance Francaise Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles