Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja, Jenerali Gaudence Milanzi amewataka Maofisa wa Mamlaka ya Wanyamapori nchini (TAWA), kutojihusisha na vitendo vya rushwa hasa uingizaji mifungo ndani ya hifadhi.
Kauli hiyo ameitoa leo kwa maofisa hao pamoja na wengine wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya mwezi mmoja kwa maofisa 90 wa TAWA yaliyofanyika Mlele mkoani Katavi.
Aidha, Meja Jenerali Milanzi amewataka maofisa hao kutumia elimu waliyoipata kutangaza vivutio vya utalii katika Mapori ya Akiba na kuelimisha jamii hata masuala ya sheria kuhusu mipaka ya hifadhi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utalii TAWA, Ikan Nkuwi aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu Dk. James Wakibara alitumia fursa hiyo kujibu ombi la wahitimu hao kuhusu upungufu wa vitendea kazi hasa magari.
“Kwa bajeti ya TAWA tumeagiza magari 60 yatakayosambazwa vituo mbalimbali kukabiliana na upungufu huo,” amesema Nkuwi.