26 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Manula: Wanasimba njooni Uwanjani na amani Jumapili

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

MLINDA mlango namba moja wa Simba, Aishi Manula, amesema ameshafahamu makosa yaliyotokea kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba, hivyo hatarajii kuona yakijirudia tena.

Simba na Yanga, zitashuka dimbani Jumapili hii, kuumana, katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, utakaochezwa  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilipokutana katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Januari 4 mwaka huu kwenye uwanja huo,  matokeo yalikuwa sare ya mabao 2-2.

Baada ya mchezo huo, Manula alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kushutumiwa na mashabiki wa Simba kuwa alifungwa mabao ya kizembe.

Shutuma za mashabiki wa klabu hiyo zilifuatiwa na benchi la ufundi la Simba linaloongozwa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbloeck  kutupwa benchi katika michezo sita iliyofuata na kumpa fursa hiyo kipa wao namba mbili, Beno Kakolanya.

Manula alirejeshwa langoni wakati wa mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Manula alisema mechi za wapinzani hazitabiriki hivyo lolote linaweza kutokea lakini wao wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanashinda.

“Siwezi kusema kuwa matokeo ya mechi ya kwanza yaliniathiri isipokuwa ni makosa ambayo yanatokea kwenye mpira na kwa sasa tumejipanga vizuri ili yasijirudie kwa mara nyingine,” alisema.

Alisema anafahamu Yanga kuna wachezaji hatari hivyo ni muhimu kuwa nao makini pale awapo langoni kwa kuokoa mikwaju itakayopigwa.

Manula aliwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi katika mchezo huo ili kutoa hamasa kwa wachezaji kutokana na ukubwa wa mechi ulivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles