25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Mangula awashukia wasaliti CCM

MangulaNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula amesema chama hicho kamwe hakitawafumbia macho viongozi wasaliti wasiokitakia mema chama hicho.
Amesema wanachama wake, wanatakiwa kuwafichua viongozi wa aina hiyo ili kukinusuru kisipoteze nafasi za majimbo na udiwani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.
“Endapo mwanachama au kiongozi, akibainika kufanya hujuma dhidi ya chama, atachukuliwa hatua kali ikiwemo ya kufukuzwa uanachama, CCM haina uhaba wa viongozi kutokana na kuwa na hazina kubwa ya wanachama wenye uwezo wa kukiongoza,”alisema Mangula.
Kauli hiyo, imetolewa baada ya kubainika kuna baadhi ya wanachama ambao wamekuwa wakijihusisha na harakati za kukihujumu ili kikose nafasi za uwakilishi.
Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, baada ya kufanya vikao vya ndani wilayani Kinondoni, Mangula alisema anashangaza kuona baadhi ya maeneo kumekuwapo na migogoro ya wanachama wenyewe kwa wenyewe.
Aliwataka makatibu wa matawi kuandaa ziara za wenyeviti wa matawi kutembelea mashina ya CCM, ili kuelezea utekelezaji wa ilani ya CCM kwa wanachama.
Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda alisema utekelezaji wa ilani ya CCM katika Wilaya ya Kinondoni umekiweka chama hicho katika nafasi nzuri ya kurudisha majimbo mawili yaliyotwaliwa na upinzani mwaka 2010.
Alisema katika kipindi cha miaka minne, majimbo hayo ambayo ni Kawe na Ubungo yamekuwa na idadi ya shule za sekondari 25, kati ya mbili zilizokuwa awali ambapo kila mwanafunzi anayehitimu elimu ya msingi anapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza.
Mafanikio hayo, yametokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na viongozi wa Serikali ya CCM, kwa kuwa wabunge wa majimbo hayo kutoka Chadema wamekuwa mstari wa mbele kupinga ujenzi wa shule za sekondari katika kata.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles