25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAMIA WAMUAGA MBUNGE BILAGO DAR

PATRICIA KIMELEMETA NA TUNU NASSOR– Dar es salaam


MAMIA ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, jana wamejitokeza katika ukumbi wa Karimjee kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilago (Chadema).

Bilago alifariki dunia Mei 26, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alipokuwa akipatiwa matibabu ya mshipa.

Mwili huo uliwasili Karimjee saa 7:06 mchana, ukitokea Hospitali ya Muhimbili ambako ulikuwa umehifadhiwa.

Baada ya kuwasili, ibada ya kumwombea marehemu ilianza.

Padre wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Magomeni, Christian Nyumayo, alisema baada ya kupewa taarifa za kumwombea marehemu, alilazimika kuwasiliana na Paroko wa Parokia ya Kakonko iliyopo mkoani Kigoma ili kujua taarifa zake na kama alikuwa anaudhuria kanisani.

“Niliongea na Paroko wa Kakonko ili nipate taarifa za marehemu, alinijibu marehemu alikuwa muumini mzuri kwenye kanisa hili, alikuwa kwenye maandalizi ya sherehe ya miaka 25 ya ndoa yake ambayo ilitarajiwa kufanyika kanisani hapo,” alisema Padri Nyumayo.

Alisema alimweleza kuwa wananchi wa jimbo lake walimwomba akafanyie sherehe zake uwanjani, yeye alikataa kwa madai anataka kufanyia kanisani.

Padri Nyumayo alisema binadamu wanapaswa kujifunza kuwa na uhusiano mzuri na wenzao kwa sababu aliwajali wananchi wake, bila ya kuangalia tofauti ya vyama.

Alisema Bilago alikuwa anajali watu wake na waumini wenzake jimboni,kila jambo linapangwa na Mungu.

 

MBOWE

Mwenyekiti wa Chadema na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, aliwashukuru wananchi waliofika eneo hilo kutoa heshima zao za mwisho.

Mbowe alisema Bilago kabla ya kufariki dunia, alimpigia simu na kumweleza matatizo aliyonayo pamoja na kumtaka kufika hospitalini hapo kumshauri.

Alisema wakati huo, alikuwa nchini Afrika  Kusini kwa majukumu mengine, na alilazimika kuwapigia simu viongozi wa chama ili wafike hospitalini na kuzungumza nae.

 Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles