24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MAMBO YANAYOSABABISHA MATATIZO WAKATI WA KUJIFUNGUA – 3

Muuguzi akimpima mjamzito.
Muuguzi akimpima mjamzito.

KATIKA makala iliyopita tulizungumzia faida za Vitamin mbalimbali ambazo zinaweza kumsaidia mama mjamzito. Tulieleza umuhimu wa madini ya ‘folic acid’ na chuma yanayopatikana katika Vitamin B.

Faida za asidi ya foliki ni pamoja na kutengeneza damu, kumkinga mtoto dhidi ya ugonjwa wa mgongo wazi na kuhakiki mfumo wa fahamu. Faida za madini ya chuma ni pamoja na kuimarisha kinga ya mwili, kutengeneza chembechembe nyekundu za damu, kuimarisha uwezo wa kuwa makini na kuongeza uwezo wa kufanya kazi vizuri.

Leo tutamalizia makala haya kwa kuangalia maandalizi ya kujifungua salama.

Utayarishe nini ili kujifungua salama?

  • Fanya utafiti mapema ili uchague kwa hekima hospitali (Kituo cha kutolea huduma za afya ambacho utajifungulia), daktari au mkunga atakayekuhudumia.
  • Mtembelee daktari au mkunga wako ili usitawishe urafiki na kuaminiana.
  • Tunza sana afya yako. Ikiwezekana tumia vitamini zinazopendekezwa lakini epuka dawa zozote isipokuwa ziwe zimependekezwa na daktari.
  • Ikiwa unapata maumivu ya kuzaa kabla ya wakati (kabla ya juma la 37) wasiliana haraka na daktari wako au hospitali utakayojifungulia.

Vitu gani utayarishe kabla ya kujifungua?

Kila mjamzito inambidi awe na vitu vifuatavyo kabla hajatimiza miezi saba ya ujauzito; vitambaa vingi visafi au khanga safi, pamba kubwa walau miligramu 500, wembe mpya (usifunguliwe mpaka unapohitajika kukata kitovu) kama huna wembe tumia mkasi safi usio na kutu (uchemshe kabla ya kuutumia), sabuni, brashi safi ya mikono na kucha.

Vingine ni vipande vya vitambaa vilivyo safi kwa ajili ya kufunika kitovu, spiriti ya kupaka mikono baada ya kuiosha, kamba mbili za nguo za kufungia kitovu au klampi mbili za kubania kitovu, sindano na uzi wa kushonea sehemu iliyochanika ya mbele na dawa ya macho kwa ajili ya mtoto.

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linashauri; “Ili kuzuia vifo vya kina mama na vichanga ni muhimu pia kuzuia mimba zisizohitajika na mimba za mapema sana. Wanawake wote ukijumlisha vijana wanapaswa kupata huduma za uzazi wa mpango, huduma za kutoa mimba salama kulingana na sheria pia kupata huduma nzuri baada ya kutoa mimba au kujifungua”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles