25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mama Ongeo na Mwanao, PCF zaungana kusaidia wanawake

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital 

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Mama Ongeo na Mwanao kwa kushirikiana na Taasisi ya Prison Charity Foundation (PCF), katika kusheherekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya zimepanga kutoa taulo za kike kwa wanawake waliopo  waliopo gerezani na kambi za waathirika wa mafuriko Hanang mkoani Manyara.

Akizungumza  na waandishi wa habari leo Disemba 12,2023 Jijini Dar es Salaam,  Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, amesema wanaunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuwawezesha wanawake kufikia ndoto zao.

Amesema wanawake waliopo gerezani wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa taulo za kike pindi wanapokuwa kwenye siku zao za hedhi.

“Kwa kutambua changomoto wanazopitia wanawake wengi walio kwenye magereza lakini pia tumeona janga lililowakuta wenzetu wa Katesh Wilaya ya Hanang  mkoani Manyara, kuna  wanawake wapo kwenye kambi wanasubiri serikali kuwawekea mazingira mazuri.

“Hivyo tutatumia muda huu kuwafikia wote magerezani na kambini Hanang kuwapelekea hizi taulo za kike,”amesema Steve Nyerere.

Pia amewataka wananchi  kujikita kwenye kusaidia jamii pindi yanapotokea majanga na si kutumia fursa hiyo kufanya mambo yao binafsi ili kujulikana. 

Naye mwanzilishi wa Prison Charity Foundation (PCF),  Josephine Lawi,amesema wameanzisha kampeni ya kumsitili mwanamke gerezeni lengo likiwa kumsaidia  taulo za kike lakini pia msaada wa kisheria ambapo hadi sasa wameshawasaidia wanawake zaidi 50  wengine wameshatoka. 

“Wamawake waliopo  gerezani wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo upatikanaji wa bidhaa za msingi za usafi pindi wanapokuwa kwenye hedhi, hivyo sisi PCF kwa kushirikiana na wadau wengine tumejipanga kuhakikisha bidhaa hizo zinawafikia yaani taulo za kike na nguo za ndani na si gerezani tu lakini tutafika kwenye kambi ya waathirika wa mafuriko Hanang mkoani Manyara,”amesema Josephine.

Ameongeza kuwa mwaka 2022 taasisi hiyo iliweza kuwafikia wanawake 376 waliopo gerezani katika mkoa Dar es Salaam,Tanga na Morogoro huku lengo likiwa kufikia magereza yote nchini.

“Kampeni hii ina lengo la kuwafikia wanawake waliopo gerezani takribani 1500 na itagharimu kiasi cha shilingi 270,000,000 ambapo gharama hiyo itahusisha ununuaji wa taulo za kike,nguo za ndani,kuchapisha,kusafirisha na kusambaza majarida yenye kutoa elimu inayohusu afya ya akili pamoja na kuongeza uelewa wa changamoto zinazowakabili wanawake na walio katika hatari ya kuingia gerezani,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles