27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mama amuua mwanawe kwa mpini wa jembe

NA RAYMOND MINJA, IRINGA

MWANAMKE mmoja, Habiba Swedi (21), mkazi wa Kijiji cha Tagamenda, Mkoa wa Iringa, amemuua mtoto wake wa miezi mitatu, Christina Kalolo kwa kumpiga mpini wa jembe.

Pia, mwanamke huyo alimjeruhi mtoto wake wa miaka saba, Grace Kalolo kwa kumpiga na mpini huo.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana asubuhi nyumbani kwa mwanamke huyo.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Baba mzazi wa watoto hao, Bosco Kalolo, aliiambia MTANZANIA, kwamba mke wake alifanya unyama huo baada ya kurukwa na akili.

“Tuliamka asubuhi vizuri tu, lakini baada ya muda mfupi, mke wangu ni kama alichanganyikiwa kwa sababu alichukua mpini wa jembe na kutaka kunipiga nao.

“Nilijizuia ili asinipige, na wakati wa purukushani nilifanikiwa kukimbia. Alipoona ameshindwa kunidhuru, aliingia ndani na kuwageukia watoto   waliokuwa wamelala kitandani.

“Nilipokuwa nje, nilisikia akipiga vitu kwa nguvu, kumbe alikuwa akiwapiga watoto kwani walianza kulia kwa sauti.

“Nilipochungulia ndani, nilimuona akiwapiga watoto kwa kutumia mpini, yaani niliumia sana kwa sababu nilijua kama nikimfuata anaweza pia akaniumiza.

“Nilipoona hali hiyo, nilikimbia kwa majirani kuomba msaada, na walipofika tulimkuta huyo mdogo ameshafariki dunia kwa sababu alikuwa amepondwapondwa kichwa,” alisema Kalolo.

Kalolo alisema yeye na majirani walishirikiana kumdhibiti mwanamke huyo kwa kumtoa nje, kisha wakaanza kuwahudumia watoto wengine wawili waliokuwa wamejeruhiwa.

“Tulipofanikiwa kumtoa nje, tulirudi ndani kwa ajili ya kuwapatia msaada watoto wengine kwa sababu mmoja kati yao alikuwa na hali mbaya kwa sababu alikuwa ameumizwa kichwani,” alisema.

Kwa mujibu wa Kalolo, ameishi na mkewe kwa miaka 10 na kufanikiwa kupata watoto wane, akiwamo Christina aliyefariki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles