TULUM, MEXICO
MWIMBAJI wa Sweden, Malin Akerman (40), amefunga ndoa na mpenzi wake, Jack Donnelly (32), katika fukwe ya Playa Playa Project uliopo jijini Tulum, nchini Mexico.
Hii ni ndoa ya pili kwa Akerman ambaye ni mwanamitindo na mwigizaji baada ya ndoa ya kwanza kufunga mwaka 2013 na mwanamuziki Roberto Zincone na baadaye kuvunjika baada ya miaka sita.
“Walionekana kuwa na furahaa pamoja baada ya kufunga ndoa walielekea katika maji ya fukwe wakifurahia uamuzi wao,” alisema rafiki wa karibu na wanandoa hao.
Oktoba mwaka huu Akerman alithibitisha kuwa katika uchumba na Donnelly.
Wanandoa hao kwa mara ya kwanza walijitokeza hadharani Machi mwaka 2017 wakati wakiwa Puerto Rico.