Brighiter Masaki
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo jumatano Julai 17, amezindua soko la kimataifa la madini na vito jijini Dar es salaam, ikiwa ni utekelezaji wa agizo alilotoa Rais Dk. John Magufuli kwa kutaka kila mkoa kuwa na soko hilo.
Akizungumza Makonda amesema uwepo wa soko hilo litasaidia wananchi kununua madini na vito halali na kupunguza matapeli waliokuwa wakiuzia wananchi na Wageni madini na vito feki.
Aidha Makonda amesema uzinduzi wa soko hilo umekuja wakati muafaka ambao Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa wakuu wa nchi za SADC ambao wataingia nchini mwezi ujao wakiambatana na wafanyabiashara amapo anaamini watapata nafasi ya kutembelea soko hilo
“Kama tunavyojuwa Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa wakuu wa nchi za SADC ambao wataingia nchini mwezi ujao wakiambatana na wafanyabiashara ambapo pia ninaamini watapata nafasi ya kutembelea soko hili” amesema Makonda.
Aidha amesema ndani ya soko hilo yanapatikana madini ya aina zote hivyo amewataka wananchi kulitumi soko hilo kwani ni halali na linatambulika na serikali.