23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda awaweka rumande maofisa ardhi

MAKONDANa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, jana aliwaweka ndani maofisa ardhi zaidi ya 10 kwa saa sita.

Imeelezwa kuwa Makonda alifanya hivyo  kwa kile kilichoelezwa kukaidi agizo lake la kuwataka wawahi katika eneo la mkutano   kusikiliza migogoro ya ardhi.

Tukio hilo lilitokea katika eneo la Nakasangawe Kata ya Wazo, Dar es Salaam, baada ya  maofisa hao kuchelewa kufika tofauti na walivyotakiwa.

Makonda alisema   walikubalina kuwahi katika kikao cha pamoja.

Alisema   lakini katika hali ya kushangaza ingawa yeye alifika katika eneo hilo kwa wakati,   maofisa hao walifika saa 5.00 asubuhi kitendo ambacho hakiendani na nidhamu ya kazi.

“Hivi sasa wamewekwa mahabusu katika Kituo cha Polisi Wazo na tumelazimika kuahirisha shughuli hii kwa muda,” alisema Makonda.

Alisema hatua aliyoichukua kwa maofisa  hao itakuwa fundisho kwa watendaji wengine   kuwafanya wawajibike wakati wote kwa ajili ya masilahi ya wananchi  na si yao binafsi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles