27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda aonya wanaokamata wapiga picha katikati ya jiji

Anna Potinus – Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza polisi wanaowazuia wananchi kupiga picha katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kama kumbukumbu za maeneo hayo kuacha mara moja ili wasaidie kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo jijini.

Makonda ameyasema hayo leo Desemba 15, 2018 jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa chaneli ya Utalii iliyopewa jina la Tanzania Safari Chanel uliofanyika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Makonda amesema kuwa sehemu maalum iliyozuiwa kupigwa picha za hivyo ni ikulu tu iliyopo Magogoni Jijini hapa.

“Inashangaza eti mtu anaona sehemu nzuri katikati ya jiji anapiga picha wanakuja wanamkamata, wasanii wanaigiza wanakamatwa,’’ anaeleza Makonda.

Hata hivyo amefafanua kuwa kwa kuwaacha watu wapige picha katika maeneo mbalimbali ya jiji hili kutasaidia kuinua utalii wa ndani na nchi kwa ujumla kama namna Marekani walivyoweza kutangaza utalii na nchi yao kwa ujumla.

“Marekani ni mfano mzuri kwani waigizaji wameifanya nchi yao kuwa ya kuvutia hadi kupelekea watu wengi watamani kwenda kuiona lakini inashangaza hapa kwetu wasanii wakienda kupiga picha wanakatazwa,” amesema Makonda.

Chaneli ya Tanzania Safari iliyoudhuriwa na viongozi mbalimbali nchini itapatika nakatika kisimbuzi cha Startimes namba 331.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles