23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Jumuiya ya Wazazi CCM kujenga shule na vyuo zaidi

Asha Bani

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dk Edmund Mndolwa amesema jumuiya hiyo haitauza shule inazosimamia, badala yake itaongeza ujenzi wa shule zaidi pamoja na vyuo vya ufundi stadi.

Hayo yameelezwa leo Desemba 15 na Dk Mndolwa wakati akieleza mafanikio ya Jumuiya hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Desemba 3 mwaka huu hafi 8.

Amesema lengo kuu ya Jumuiya hiyo ni kuhakikisha wanaongeza idadi ya shule badala yakuziuza, pia jumuia hiyo imepanga kufanya miradi mbalimbali ya kukuza uchumi wanchi.

“Katikakipindi cha mwaka mmoja Jumuiya pamoja na mambo mengine imejiwekea malengo ya kujiendesha ikiwa ni pamoja na kuboresha shule na vyuo vyake, kuanzisha miradi mipya ya kiuchumi (mradi wa ufugaji nyuki), kufanya kazi ya siasa na kuiimarisha CCM kwa kufanya ziara mbalimbalj za kukagua uhai wa chama hicho,” amesema Dk Mndolwa.

Dk. Mndolwa ameongeza kuwa tayari wilaya zote nchini imeagizwa kuanzisha miradi ya nyuki katika shule zake na tayari mpaka sasa walimu 44 wameshapatiwa mafunzo yamradi huo.

“Katika kuhakikisha jamii inakua katika maadili, kila mtanzania anakuwa mstari wa mbele kuweka mkazo ili matumizi ya utandawazi yawe ya kujenga na si kutumika vibaya kwa jamii,” amesema Dk Mndolwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles