22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, June 22, 2024

Contact us: [email protected]

Makombe Yanga yapamba banda la NMB sabasaba

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

MASHABIKI wa Yanga leo Julai 7,2023 wamepata fursa ya kupiga picha na makombe ya ubingwa ya timu yao katika banda la Benki ya NMB kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mauzo na Mtandao wa watawi wa benki hiyo, Donatus Richard amewaomba wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuchangamkia fursa ya kujisajili ili kupata kadi za uanachama ambazo zitawasaidia kutambulika na klabu pamoja kupata kwa urahisi huduma za kibenki.

“Tunaomba mashabiki wa Yanga na wanachama wajitokeze kwa wingi siku ya Jumatatu tarehe 10 mwezi huu kwenye matawi yetu kwa ajili ya kufanya usajili pamoja na kulipa ada zao.Matawi yetu nchi nzima yamejipanga vizuri kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kirahisi,” amesema Richard.

Akizungumzia nafasi waliyopata shabiki wa Yanga, Mary Jakobo amesema amefurahi kupiga picha na makombe ya timu yao waliyotwaa msimu wa 2022/2023 huku akitamba kuwa msimu ujao lazima wabebe kwa mara nyingine.

“Nimefurahi kupata nafasi ya kupiga picha makombe yetu msimu ujao naamini tutaendelza ushindani na kutete makombe yetu yote,”amesema Mary.

Naye Doto Kapela amesema msimu huu timu yao inafanya usajili mzuri ambao utawapa mafanikio makubwa msimu ujao utakaoanza mwezi Agosti mwaka huu.

Yanga inatarajia kusajili zaidi ya wanachama milioni nane kwa miaka miwili ya mkataba huo na NMB walioingia makubaliano wiki iliyopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles