26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

MAKINDA ATAKA WAKULIMA KUTOTEGEMEA RUZUKU

Na JANETH MUSHI-ARUSHA

 

SPIKA wa Bunge Mstaafu, amewataka wakulima nchini kuachana na kilimo cha mazoea kinachotegemea ruzuku kutoka serikalini.

 

Badala yake, amewataka wakulima hao kujiwekea akiba kwa ajili ya kununua pembejeo za kilimo.

Kauli hiyo aliitoa juzi, alipokuwa akizungumza na wakulima katika Maonyesho ya Wakulima na Wafugaji ya Nanenane, Kanda ya Kaskazini, yanayoendelea katika viwanja vya Themi, jijini hapa.

Makinda alisema kuwa, wakulima wengi wamekuwa wakitegemea ruzuku kutoka serikalini ambayo pia huwa haitoshi, jambo linalorudisha nyuma wakulima wengi na kushindwa kubadili maisha yao kupitia kilimo.

 

“Pembejeo ni changamoto kwa wakulima, mimi siyo muumini sana wa ruzuku, ndiyo maana naona inatakiwa mkulima mwenyewe ajipange vizuri anapokuwa katika kilimo.

 

“Lazima mkulima ajifikirie, kwamba amelima mwaka huu na amepata mazao fulani na alipolima mwaka jana alitumia mifuko mitatu ya mbolea na mapato aliyopata ayawekee akiba ya fedha za mifuko mitatu ya pembejeo kwa mwaka unaofuata.

 

“Uzoefu wangu na ruzuku unaonyesha kwamba, unapofika wakati wa ruzuku ukipewa mfuko mmoja wa mbolea, hautakusaidia.

 

“Lazima wakulima wajifunze kuweka akiba ili kuepuka tabia ya kugombea mfuko mmoja wa ruzuku, kwa sababu hiyo ni dalili ya kurudi nyuma kimaendeleo na inaleta umasikini zaidi badala ya kukupa maendeleo,” alisema Makinda.

 

Alitaja changamoto nyingine inayowakabili wakulima kuwa ni pamoja na taasisi za fedha kushindwa kuwapa wakulima mikopo kwa wakati wanaoihitaji.

 

Kuhusu mabadiliko ya tabianchi, kiongozi huyo alisema wakulima nchini wana wajibu wa kuwatumia wataalamu wa hali ya hewa ili wanapolima, wajue hali ya hewa kwa wakati husika itakuwaje.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles