27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Makatibu Wakuu SADC wakutana kwa dharura kujadili hali ya ulinzi DRC

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Samwel Shelukindo ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Kamati ya Utatu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Balozi Shelukindo ameshiriki katika Mkutano huo akiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano umejadili hali ya ulinzi na usalama mashariki mwa DRC.

Mkutano huo umefuatiwa na Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC MCO) ambapo ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo umeongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba (Mb.)

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles