27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Makamu wa Rais : Acheni kutegemea mvua, jikiteni katika umwagiliaji

                       Bethsheba Wambura

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka  wakulima na wadau wa kilimo kuacha kutegemea maji yatokanayo na mvua badala yake wajikite katika umwagiliaji wa mazao, kuendana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuifanya sekta hiyo kuwa na tija.

Makamu  wa Rais ameyasema hayo leo Jumamosi Novemba 3, alipokuwa akizindua tamasha la mvinyo uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa jijini Dodoma ambapo amesema kilimo cha Tanzania kwa sasa bado kinategemea mvua mnazo zinaweza kumwagilia hekta 461326 pekee ikilinganishwa na hekta Milioni  29 ambazo zingeweza kumwagiliwa endapo tu wakulima watafanya kilimo cha umwagiliaji.

Amesema kaulimbiu ya tamasha hilo inayosema ‘hamasisha matumizi ya zabibu za Tanzania kwa ukuaji wa viwanda vyetu’ inayendana na dhima ya serikali ya kujenga Tanzania ya viwanda vitakavyozalisha bidhaa kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini na kuuuzwa ndani na nje ya nchi.

“Utafiti uliofanywa mwaka 2011 kwa ushairikiano na wadau wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi  unaonesha kuwa gharama ziletwazo na mabadiliko hayo kwa  Tanzania  zinazidi asilimia Moja  ya pato la mwaka la taifa.

“Ikiwa  pato la taifa  hilo  linatokana na shughuli nyingi ikiwemo kilimo zinazoathiriwa moja kwa moja na mabadiliko ya tabia nchi naendelea kusisitiza upandaji wa  miti ili kupunguza athari za mabadiliko hayo na kupunguza mmomonyoko wa udongo lengo ikiwa likiwa  kutunza mazingira kwa kizazi cha sasa na baadae, “amesema.

Aidha Samia ametoa rai kwa wakulima, watafiti ,wasindikaji na wasambazaji kubadilika kutoka katika kilimo cha kujikimu hadi kilimo cha biashara kwa kufuata kanuni za kilimo zenye kuongeza tija katika mazao na kuzingatia matumizi sahihi ya dhana za kilimo na pembejeo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles