Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman leo Jumamosi Septemba 30, ametembelea banda la Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) katika maonesho ya sita ya teknolojia ya madini Geita na kupata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mgodi huo.
Pia amepata maelezo kuhusu huduma za uchunguzi na elimu ya saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume zinazotolewa na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita kwa ushirikiano wa GGML ambapo hadi Septrmba 29, zaidi watu 1,000 wamefanyiwa vipimo.
Akitoa maelezo kwa Makamu Rais huyo wa Zanzibar ambaye ndiye mgeni rasmi anayefunga maonesho hayo yaliyofanyika kwa siku 10, Meneja Mwandamizi wa GGML anayeshughulikia mahusiano ya jamii, Gilbert Mworia alisema kampuni hiyo ndio inayoongoza kwa kuwa muajiri bora nchini.
Pia inaongoza kuwa kuzingatia sheria ya local content Pamoja na kuzingatia masuala ya usalama kazini.
Pamoja na mambo mengine amesema GGML ambaye ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo yaliyoanza tarehe 20 Septemba mwaka huu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong amemshukuru Makamu huyo wa Rais kwa kutembelea banda hilo na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali.