23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 11, 2024

Contact us: [email protected]

Makala: Mkoa wa Lindi unavyodhibiti Surua kwa Watoto

*Ni kwa kuzingati ratiba ya chanjo mapema

*Wazazi waendelea kuhamasika

Na Hadija Omary, Lindi

Surua ni miongoni mwa magonjwa ya kuambukiza yanayotisha kwa binadamu. Huu ni ugonjwa ulio na kiwango cha juu cha karibu asilimia 100 cha mashambulizi pindi mtu apatapo vimelea vya ugonjwa huu.
 
Kulingana na tafiti mbalimbali, ugonjwa huu unaosababishwa na virusi jamii ya paramyxovirus unaweza kumpata mtu wa rika lolote ila huathiri zaidi watoto.

Dalili

Dalili za awali za surua ni koo kuuma, kikoozi, homa na madoa ya rangi ya kijivu au nyeupe kwenye sehemu ya ndani ya mashavu. Baada ya siku chache, upele mwekundu hutokea.
 
Pamoja na kuwepo chanjo ya ugonjwa huu, bado surua ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo vingi vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano katika baadhi ya maeneo duniani hasa kwa nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania.

Ugonjwa huu ambao ulitoweka katika baadhi ya nchi, umeanza kuonekana tena hivi karibuni miongoni mwa watu ambao hawakupata chanjo katika nchi mbalimbali barani Ulaya ikiwamo Uingereza na nyingine za Bara la Afrika ikiwamo Kenya na Tanzania.
 
Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia watoto, (UNICEF) na la afya duniani (WHO) yamesema idadi ya wagonjwa wa surua duniani kwa miezi miwili ya mwanzo ya mwaka 2022 iliongezeka kwa asilimia 79 kulinganisha na kipindi kama hicho mwaka 2021 na hivyo kuwa ni mazingira yanayoweza kuchochea mlipuko wa ugonjwa huo unaozuilika kwa chanjo.
 
Mashirika hayo yanabainisha kuwa, mvurugiko wa utoaji chanjo unaohusishwa na milipuko mingine ya magonjwa, ongezeko la ukosefu wa usawa katika kupata chanjo na kuelekezwa kwa rasilimali kutoka ratiba za chanjo za kawadai kunasababisha watoto wengine kusalia bila kinga dhidi ya surua na magonjwa mengine yanayozuilika.
 
Mratibu wa chanjo Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Joyce Mchopa anasema ugonjwa huo wa surua hauna tiba maalum ingawa kupumzika na kunywa maji ya kutosha ni muhimu sana ambapo homa inaweza kudhibitiwa kwa dawa ikiwa inamfanya mtu kujihisi mgonjwa.

“Watu wenye surua wanaweza kuwaambukiza wengine wanapoanza kuwa na dalili za awali  siku 3 – 4 baada ya upele kutokeza. Watu wengi wenye surua hupata nafuu ndani ya wiki moja toka dalili za awali kujitokeza.
 
“Kukamilisha dozi za chanjo kwa mtoto kunamlinda dhidi ya surua ambapo dozi mbili za surua zinamkinga mtoto kwa ufanisi wa karibu asilimia 97 katika kuzuia surua ikiwa ameathiriwa na virusi.

“Dozi moja ni karibu asilimia 93, huku akieleza kuwa dozi ya ugonjwa huo utolewa kwa awamu mbili awamu ya kwanza utolewa kwa mtoto wa miezi tisa na dozi ya pili hutolewa kwa mtoto anapotimiza miezi 18 sawa na na mwaka mmoja na miezi sita,” anasema Joyce.
 
Anasema halmashauri hiyo ya Ruangwa kwa mwaka 2023 inalengo la kutoa chanjo kwa Watoto 4,643 ambapo mpaka sasa uchanjaji wa chanjo ya kwanza tayari wameshawafikia jumla ya watoto 2,756 sawa na asilimia 90 huku dozi ya pili wakiwa wameshawafikia watoto 2,556 sawa na asilimia 53.
 
Ili kuhakikisha watoto wote walio na umri wa kupata chanjo wanakamilisha ratiba zao za chanjo swala la ufuatiliaji ni jambo linalopewa kipaumbele.

Zainab Shabani ni Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Ruangwa Mjini ambaye anasema kwamba wanalazimika kuweka vibandiko kwenye kadi ya kliniki ya mtoto kama alama pale ambapo anapata dozi ya kwanza kwa tarehe na mwezi husika.
 
Anasema ikitokea mtoto amekosa kupata chanjo ya surua baada ya kutimiza miezi tisa ama zaidi mtoto huyo uanzishiwa chanjo hiyo mara tu baada ya kufahamika kama hajapatiwa japo utolewaji wake utakuwa ni tofauti na watoto wengine.
 
“Iikitokea mtoto ataletwa kituoni na tukagundua hajapata chanjo kabisa kama atakuwa na umri usiozidi miezi 18 atapatiwa dozi ya kwanza muda huo alafu atarudi tena kupata dozi ya pili baada ya kutimiza miezi 18 na endapo atakuwa amevuka umri wa miezi 18 atapata dozi ya kwanza siku hiyo kisha atalazimika kupata dozi ya pili na baada ya mwezi mmoja atapata dozi ya pili.           
 
Ingawa baadhi ya wagonjwa hupona katika kipindi cha siku 10 mpaka 14, baadhi hupata matatizo zaidi yanayoweza kuwa ya muda mrefu.
 
Mratibu wa Elimu na Uhamasishaji namna ya kujikinga na magonjwa Dk. Ernest Mtauka anasema matatizo hayo ni kama maambukizi njia ya masikio (Otitis media), uambukizi kwenye mirija ya hewa ya koo (bronchitis) maambukizi kwenye njia ya sauti (laryngitis) na croup.

Kulingana na maelezo yake, surua inaweza kusababisha kuvimba katika sehemu ya sauti na kuathiri uwezo wa kutoa sauti lakini vilevile inaweza kusababisha uvimbe katika kuta za utando wa njia ya hewa.
 
Anaeleza matatizo mengine kuwa ni maambukizi katika njia ya chini ya mfumo wa hewa kama vile homa ya mapafu (pneumonia) ambayo ni sababu kuu inayosababisha vifo vinavyotokana na surua.

“Mgonjwa wa surua ni rahisi kupata homa ya mapafu kwa sababu kinga ya mwili wake huwa imepungua. Homa hii ya mapafu yaweza kusababishwa na aina nyingine ya virusi kama adenovirus, herpes simplex au bakteria kama Staphylococcus aureus, Streptococcus pneumonia, Haemophillus influenza, Klebsiella pneumonia. Lakini vilevile kifua kikuu kinaweza kutokea kwa kusababishwa na upungufu huu wa kinga mwilini,” anasema Dk. Mtauka.  

Kulingana na Dk. Mtauka, surua pia inaweza kusababisha utapiamlo kwa sababu ya ukali wake hasa kwa watoto ambao hawapati lishe nzur, hiyo ni kutokana na kwamba inahusishwa pia na kuharisha na kutapika na kusababisha upungufu wa maji mwilini.

“Surua husababisha upungufu wa Vitamini A na kusababisha tatizo la kutoona vizuri ambalo hujulikana pia kama Keratitis. Kwa mtoto ambaye ana upungufu wa Vitamini A tatizo la macho huwa kubwa zaidi na kwa kitaalamu hujulikana kama Keratomalacia ambapo sehemu nyeupe ya jicho hutoboka,” anasema Dk. Mtauka.

Hata hivyo, licha ya msisitizo wa utolewaji wa chanjo hizo pamoja na mikakati ya kuwafikia Watoto wote walio na umri wa kupata chanjo lakini bado baadhi ya wazazi hawana uwelewa wa kutosha juu ya ugonjwa wa surua licha ya kukiri kuwapeleka watoto wao katika vituo vya kutolea huduma kupata chanjo hizo.
 
Aziza Saidi ni Mama wa mtoto mmoja mwenye umri wa miezi 10 ambaye anasema kuwa mtoto wake amepatiwa chanjo ya surua akiwa na umri wa miezi 9 na ameambiwa anatakiwa kumpeleka tena mtoto wake pindi atakapofikisha umri wa miezi 18.

“Mimi ninachofahamu ni kwamba chonjo zinazotolewa na wataalamu wa afya zinamlinda mtoto na magojwa, hivyo nitafanya hivyo pindi muda utakapowadia kulingana na maelekezo ya wataalamu,’ ana

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles