29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Makampuni yatakiwa kutoa ajira kwa Vijana nchini

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Ujenzi, Godfrey Kasekenya, ameyataka makampuni mbalimbali kutoa ajira kwa vijana kukamilisha kauli ya Rais John Magufuri ya Tanzania ya viwanda.

Akizungumza mapema leo Januri 14, jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa ujio mpya wa magari ya Isuzu, Kasekenya, amesema kuwa ujio huo umekuja kwa wakati sahii kwa sababu utaongeza ushindani katika biashara na pia utaongeza ajira kwa watanzania.

“Naamini bidhaa zenu zitakuwa za kawaida kwa watanzania, na pia utaongeza ajira kwa vijana wakitanzania ili waendelee kupata ujuzi kutoka kwenu na ninyi kujifunza kupitia wa,” amesema Kasekenya.

Pia amesema anaamini watakuwa moja ya chachu katika kuimarisha suala la taarifa kwa umma kupitia bidhaa zenu zitakazo nufaisha taifa letu.

Kwa upande wake Meneja Direkta, Deogratius Kisindi, amesema kuwa kampuni ya magari ya Isuzu ilipotea kwa muda wa miaka mitatu kwa changomoto tofauti kupitia changamoto hizo wamejipanga na kurudi tena.

“Kikubwa ni kuwapatia watanzania bidhaa nzuri na bora zitakazodumu kwa muda mrefu kwa bei nafuu, na kutokosa tena bidhaa ya Isuzu” amesema Kisindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles