*Akubali kuongeza muda wa malipo
Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital
RAIS Dk. Samia Suluhu ameridhia kupunguza gharama na kuongeza muda wa manunuzi ya nyumba za Magomeni kota kutoka miaka 15 hadi 30 ikijumuisha na miaka 5 ya kukuaa bure.
Akizungumza leo Mei 8, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA), Arch. Daudi Kondoro amesema lengo la mkutana huo ni utaratibu wa mauzo ya nyumba za Magomeni kota zilizogawaiwa kwa wakazi 644.
“Rais Dk. Samia amepunguza gharama kwa wanunuzi bila kuzingatia gharama za thamani ya ardhi pamoja na vingine amefanya punguzo kubwa sana kutoka billion 52.2 hadi bilioni 18.2 za nyumba Magomeni kota,” amesema Arch. Kondoro.
Arch. Kondoro amesema nyumba hizo zitauzwa kwa nyumba ya chumba kimoja Sh milioni 48.5 na nyumba ya vyumba wiwili Sh milioni 56.8 zote zitalipwa kwa awamu kwa muda wa miaka 30.
Amesema kabla ya hapo nyumba ya chumba kimoja ilikuwa inauzwa Sh milioni 74.8 na vyumba viwili Sh milioni 86.
Amesema kimsingi wana mktaba wa miaka 30 imetolewa unafuu kama mnunuzi anaweza kulipa kabla ya miaka 30 inaruhusiwa na kulipa kwa awamu inaruhusiwa pia.
Aidha, amesema ambao watakuwa tayari na kuonyesha nia kwa ajili ya kununua nyumba hizo ndani ya siku 14 TBAinatoa nafasi.
“Nyumba zilizozinduliwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa zimejengwa maalumu kwa ajili ya watumishi wa umma. zinatarajiwa kuanza kutumika Juni 1, mwaka huu ambapo zitapangishwa Sh 870,000 kwa mwezi,” amesema Arch. Kandoro.