32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Makala: Handzdown Records kutoka Marekani ilivyomuibua rapa Trixy Tonic

Na Christopher Msekena, Mtanzania Digital

Miongoni mwa Rapa wa Kike wanaokuja kwa kasi hapa Bongo ni Trixy Tonic, Mrembo ambaye yupo chini ya usimamizi wa Handzdown Records & Label yenye makazi yake nchini Marekani.

Trixy amefanya mahojiano yafuatayo na www.mtanzania.co.tz ili mashabiki waweze kumfahamu vizuri yeye na harakati zake za muziki wa Hip hop.

SWALI: Trixy Tonic ni nani?

Trixy: Jina langu halisi ni Aneth Godson a.k.a Trixy Tonic mimi ni msanii wa kike ninayefanya muziki wa Hip hop na hili jina limetokana na utundu utundu wakujua mambo mengi na ubunifu mkubwa, vile vile mimi ni mwanadada ninayejituma na msomi wa Chuo Kikuu pia ni mfanyabiashara wa nguo na vinywaji na ni mpambanaji ambaye sichoki ila nimejaa upendo na ninapenda mafanikio.

SWALI: Ukiwa Rapa wa kike unapitia changamoto gani kwenye muziki?

Trixy : Kama rapa wa kike changamoto ninazopitia ni namna ya kusambaza kazi zangu kwani wakati mwingine inakuwa vigumu sana maana kunakuwa na uhitaji mkubwa wa fedha, lakini pia changamoto ya rushwa ya ngono huwa ni kikwazo kikubwa kwangu na katika kufanya muziki wangu.

SWALI: Kwanini ulichagua kufanya rap na sio muziki mwingine?

Trixy: Niliamua kufannya rap kwasababu napenda sana Hip hop na huwa nakuwa huru zaidi katika kuweka wazi hisia zangu za mambo mbalimbali yanayozunguka jamii yetu. Pia ni kipaji nilichopewa na Mungu maana kurap kama mtoto wa kike si wengi wanaweza kufanya hivyo ila mimi nimebarikiwa namna ya kujua ‘kuflow’ vizuri.

SWALI: Rapa gani walikuvutia kufanya Hip hop?

Trixy: Marapa walionivutua kufanya rap ni Remy Ma na Nicki Minaj. .Nicki Minaj akiwa zaidi kwasababu nilikuwa naona anajua kwenye midondoko yake vile vile kwa sababu nimezaliwa nae tarehe moja na mwezi mmoja amenizidi mwaka tu kwahiyo ni kama dada yangu na huwa naona ipo siku nitakuja kumrithi na Dunia nzima muziki wangu ninaoutoa.

SWALI: Ulipata vipi nafasi ya kusimamiwa na lebo ya Handzdown kutoka Marekani?

Trixy: Nafasi hii niliipata kwa kupitia Prodyuza KITA anayefanya ngoma za Kikosi Kazi, yeye amekuwa kama kaka yangu na mtu anayenipa ushauri katika kukuza muziki wangu.

Yeye ndio aliniunganisha na CEO wa Handzdown Record ambapo walishawahi kufanya kazi pamoja kipindi cha nyuma, hivyo Handzdown Records ilihitaji kupata msanii watakayeweza kufanya nae kazi katika lebo yao ndipo kaka Kita aliwatumia kazi zangu na kuona nafaa, mwisho wa siku nikasainiwa Handzdown Records iliyopo Marekani kwa sasa.

Namshukuru CEO na Mwanzilishi wa Handzdown Records anaitwa Cyprian Obed a.k.a DJ Sippytac na makao yake yapo Dallas, Texas pia nimesainiwa kwa mkataba wa miaka mitano ambapo tutatoa EP mmoja kila mwaka na albamu tatu na hapa nilipo nasubiri kukamilisha mkataba wangu.

SWALI: Mipango yako kwa sasa ni ipi kwenye muziki?

Trixy: Mipango yangu ni kuhakikisha nafasi niliyopewa na kuipata kama bahati ni kufanya kwa ukamilifu kufanya kazi kubwa na wasanii mbalimbali wa Marekani, Tanzania na duniani kote.

Kwa ujumla kuhakikisha nawakilisha nchi yangu Tanzania vizuri duniani kote kama msanii Bora wa Kike anayefanya Hip hop pia nimeachia video ya ngoma yangu mpya inaitwa Nicheki, kila mmoja anaweza kuingia YouTube na kuitafuta ili aone uwezo mkubwa nilioufanya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles