30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]

Maji ya Ziwa Victoria kumaliza uhaba wa maji Simiyu

NA Samwel Mwanga,Simiyu

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kuanza kutekeleza kwa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria utaondoa changamoto ya upatikanaji wa Maji katika mkoa wa Simiyu.

Mkoa wa Simiyu unatekekezwa Mradi Mkubwa wa Maji kutoka Ziwa Victoria wa mabadiliko ya tabianchi.

NAIBU Katibu Mkuu,Wizara ya Maji, Cyprian Luhemeja(mwenye kofia)akiongea na baadhi ya Wakandarasi wa Kampuni ya CCECC ya nchini China inayotekeleza Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria katika mkoa wa Simiyu.

Amesema hayo mara baada ya kutembelea eneo la Nyashimo katika wilaya ya Busega ambapo kuna chanzo cha maji na mahali ambapo patajengwa mtambo wa kutibu na kuchuja Maji kupitia mradi huo.

Luhemeja amesema kuwa mkoa wa Simiyu maeneo makubwa ni hali ya ukame hivyo hali ya upatikanaji wa vyanzo vya Maji ni tatizo hivyo kuanza kwa Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria ndiyo suluhisho la upatikanaji wa Maji katika mkoa huo.

“Mkoa wa Simiyu maeneo makubwa ni hali ya ukame hivyo maji yako chini sana kwa msingi huo Mradi huu wa Maji haya ya Ziwa Victoria ndilo litakuwa suluhisho pekee la upatikanaji wa Maji safi na salama katika mkoa wa Simiyu,” amesema.

Amesema serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 440 kwa ajili ya utekekezaji wa mradi huo kwa kipindi cha miaka miwili kupitia Kampuni ya CCECC ya nchini China.

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Mhandisi Cyprian Luhemeja(wa kwanza kushoto)akiangalia ramani ya Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria mkoani Simiyu katika eneo la Nyashimo wilayani Busega mkoani humo.

Pia, ameitaka kampuni hiyo inayotekeleza Mradi huo kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha inamalizika kwa wakati ili Wananchi waweze kupata maji safi na salama.

Mhandisi Luhemeja pia ameiagiza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA) mkoa wa Simiyu kuhakikisha kuwa miundombinu yote ya maji iliyopo kwenye mkoa huo ambapo Bomba kubwa la maji hayo ambalo litapita kwenye maeneo hao iunganishwe ili itumike kusambaza maji kutoka Ziwa Victoria.

Awali, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Simiyu, Mariamu Majala amesema kuwa kwa sasa hali ya upatikanaji wa maji katika maeneo ya vijijini katika mkoa huo ni asilimia 71 na kwa mwaka huu wa fedha jumla ya miradi 29 ya maji itatekelezwa kwa lengo la kumtua mama ndoo kichwani.

Mhandisi Majala amesema kuwa kwa ukubwa wa tatizo la upatikanaji wa maji katika mkoa huo wanaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu kwa kuendelea kuwapatia fedha pamoja na mtambo Mkubwa wa kuchimba visima vya Maji ili kupunguza changamoto hiyo.

“Tunaishukuru sana serikali kuendelea kutupatia fedha nyingi za kutekeleza miradi mbalimbali ya maji na sasa tuna gari kubwa lenye mtambo wa kuchimba visima virefu ambalo limenunuliwa na serikali na lengo ni kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika mkoa wetu wa Simiyu,”amesema Mhandidi Majala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles