25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Majeruhi yaitesa Tottenham

LONDON, ENGLAND

TIMU ya Tottenham inakabiliwa na hatari ya kumkosa Dele Alli Alhamisi wakati ikivaana na Chelsea katika mchezo wa Kombe la Ligi, utakaochezwa Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Alli alipata  jeraha la nyama za paja juzi usiku wakati akiwa katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi Fulham ambao Tottenham ilishinda mabao 2-1.

Katika mchezo huo, Alli alikuwa akitumika kama mbadala wa Harry Kane ambaye anasumbuliwa na majeruhi ya  kifundo cha mguu  ambayo yatamweka nje ya uwanja hadi Machi mwaka huu.

Alli anaweza kuungana na Kane ikiwa vipimo atakavyopimwa leo vitaonyesha kuathirika zaidi na tatizo hilo na iwapo hali itakuwa hivyo Tottenham itakabiliana na kipindi kigumu katika safu ya ushambuliaji.

Wakati  washambuliaji hao wawili wakikumbwa na tatizo la majeruhi, mshambuliaji mwingine, Son Heung-min, ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Korea Kusini ambayo inashiriki michuano ya Kombe la Asia.

Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino, alisema: “Tunatakiwa kuendelea kuchunguza tatizo lake lakini  maumivu yapo katika misuli ya paja na tunahitaji kuwa makini katika jambo hili. Amekuwa  akilalamika sana kuhusu paja lake, yupo katika hali mbaya sana.

“Huwezi kuwa tayari kumsikiliza au kumwangalia wakati akiugulia.”

Tayari Kane ataikosa  mechi ya nusu fainali ya Kombe la Ligi pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund, pia mchezo wa hatua inayofuata Kombe la FA pamoja na Ligi Kuu dhidi ya  Chelsea na Arsenal.

Kutokana na hali hiyo, Pochettino amesisitiza kuwatumia  wachezaji wengine kama vile, Lucas Moura, wakati Moussa Sissoko  akiwa  hana uhakika na afya yake.

“Hakuna hofu,” alisema Pochettino akikisitiza upana wa kikosi chake.

“Hali hii inatoa nafasi kwa wachezaji wengine kuonyesha kiwango chao. Tunakwenda kucheza dhidi ya Chelsea tunatarajia kushinda mchezo huo, ni jambo muhimu kwetu. Moura yupo tayari kwa mapambano  akitokea benchi au kikosi cha kwanza.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles