27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mtumishi Tanroads kizimbani kwa tuhuma za rushwa

Na PENDO FUNDISHA-MBEYA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Mbeya, imemfungulia kesi mtumishi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa tuhuma za kupokea hongo ya Sh 597,000.

Kesi hiyo namba CC. 189/ 2018, imefunguliwa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, chini ya kifungu cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 dhidi ya mtumishi huyo,Zabron Kenan.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Kiyabo  alisema mtumishi huyo akiwa msimamizi wa mzani wa kupima magari uliopo eneo la Uyole jijini Mbeya, alipokea kiasi hichokutoka kwa mtumishi wa Kampuni ya China ya Chongqing Foreign Trade Economic Corporation.

Alisema  mtumishi wa Kampuni ya Kichina, Onesphory Ngonyani, inasemekana alitoa kiasi hicho ili gari aina ya Howo lenye namba za usajili T 755BZC na tela namba T587BPY lililokuwa halina kibali cha mzigo wenye upana usio wa kawaida (abnomal wide loard), lipite kwenye mzani huo bila ya kukamatwa.

“Taarifa zilifika ofisini na kuweka mtego ambapo ofisi ilifanikiwa kumtia nguvuni mtumishi Novemba  25, 2018 na kumfikisha mahakamani  Novemba 30.2018 ambapo alifunguliwa kesi ya jinai ‘’alisema.

Alisema, tasisi hiyo inaendelea kumtafuta mtumishi wa kampuni hiyo, Onesphory Ngonyani kwani alifanikiwa kutoroka baada ya kutoa hongo hiyo, huku gari lake aina ya Toyota Carina lenye namba  T108 BQH likishikiliwa na ofisi hiyo ya taasisi hiyo.

Alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa gari hiyo, iliponunuliwa haikubadilishwa umiliki wake hivyo kuna fedha ya serikali inatakiwa kulipwa kama ada ya kuhamisha umiliki na endapo ataendelea kujificha chombo hicho cha moto kitapigwa mnada ili kufidia gharama za serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles